Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo wa
Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja
---
Na MWANDISHI WETU
JESHI la Polisi nchini kuwachulia hatua
kali kwa watu ambao watahujumu zoezi la sensa ya Watu na Makazi
inayotarajiwa kuanza Agasti 26 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa
habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo wa
Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jeshi limejipanga
katika kuhakikisha zoezi la sensa linafanyika katika hali utulivu
pasipokuwepo na uvunjifu wa amani wa kutaka kuhujumu zoezi hilo.
Chagonja alisema kuwa watu ambao watafanya
uhalifu ikiwemo kuchana karatasi za makarani wa sensa watachuliwa
hatua kwa kuwafikisha mahakamani kutokana na sheria ya sensa.
Alisema kwa kususia sensa ni kosa ambapo
aliwataka wenye malalamiko kutekeleza zoezi katika hali usalama na
baadaye baada ya kazi hiyo kukamilika ndio wafuatilie madai yao.
“Jeshi halitaweza kuwaacha watu ambao
wanataka kuhujumu zoezi la sensa ambalo liko kisheria kwa madai yao
wanatumia taasisi katika kushawishi wananchi wasijitokeze katika
zoezi ambalo watendaji wetu wametekeleza hadi kufikia hapo”.alisema
Chagonja.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Makosa ya
Jinai Robert Manumba alisema kuwa tayari jeshi la polisi
linawashikilia watu kutokana na kutaka kuhujumu zoezi hilo.
Alisema bado wanaendelea kufuatilia kwa
karibu juu ya watu ambao wanashawishi wananchi kugoma katika
kuhesabiwa kwa sababu zao ambazo haziko kisheria.
Manumba
aliwataka wananchi kushirikiana kwa kutoa taarifa za watu ambao
wanaopita kwa kubandika sitika katika nyumba juu ya kugomea sensa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)