Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (katikati)
akizungumza wakati wa hafla ya makabidiano ya hundi yenye thamani ya
shilingi 5m/- kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha
wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC. Kulia ni na Kaimu
mkurugenzi wa hospitali Profesa Raimos Olomi na kushoto ni mkurugenzi
wa utawala wa hospitali hiyo Stanley Mmbaga
Kaimu
mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC rofesa Raimos Olomi akiifurahia
hundi ya shilingi 5m/-iliyotolewa na Benki ya KCB kusaidia ununuzi wa
vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya
KCMC. Kushoto ni Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau
Meneja
wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (katikati) akizungumza
na Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC {kushoto} Profesa Raimos
Olomi na Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya akina mama Dkt Gileard Masenga
(kulia) mara baada ya kutoa msaada wa 5m/- kusaidia ununuzi wa vifaa
katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo.
Meneja
wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (kushoto) akimkabidhi
mfano wa hundi ya shilingi 5m/- mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake wa
hospital ya KCMC Dr Gileard Masenga. Fedha zilizotolewa zinalenga
kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi
katika hospitali. Katika kati ni Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya
KCMC Profesa Raimos Olomi
Meneja
wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau akimkabidi mfano wa
hundi ya shilingi 5m/- kwa Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC
{kulia} Profesa Raimos Olomi kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa vifaa
katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC.
Mkuu
wa idara ya magonjwa ya wanawake wa hospital ya KCMC Dr Gileard Masenga
akitoa maelezo kwa Emmanuel Grayson ambaye ni mkuu wa masuala ya
kijamii wa Benki ya KCB tawi la moshi juu ya wodi iliyokarabatiwa na
benki hiyo mwaka jana mara baada ya kutoa msaada wa wa 5m/- kusaidia
ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika
hospitali hiyo.
---
Na Mwandishi Wetu
Benki
ya ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa shilingi milioni tano (5m) kusadia
ununuzi wa vifaa katika wodi ya akina mama katika hospitali ya rufaa
KCMC ikiwa ni jitihada za kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika kwa akina
mama wajawazito,
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya hundi ya fedha hizo uliofanyika hospitali
hapo jana, Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau
alisema kuwa msaada huo ulikuwa ni muendelezo wa msaada ambao benki hiyo
iliutoa mwaka jana.
Mwaka
jana tulikarabati chumba cha akina mama wagonjwa hatuti kwa gharama ya
zaidi ya shilingi milioni kumi na moja. Nilipofamishwa kuwa chumba
kilikuwa tayari lakini hakuna vifaa niliona kuna umuhimu kutoa msaada wa
kununulia vifaa ili pesa iliyotolewa kwanza isiwe imepotea bure,”
alieleza
Meneja
huyo wa tawi alisema kuwa Benki yake imeamua kutoa msaada huo kwa
kutambua umuhimu wa kusaidia serikali katika kupunguza vifo vya mama na
mtoto na kuhakikisha kuwa malengo ya millennia ya kuhakikisha kuwa vifo
vya akina mama na mtoto vinakwisha kufikia mwaka 2015.
Akipokea
msaada huo, Kaimu mkurunzi wa hospital ya KCMC Profesa Raimos Olomi
alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza vifo vya akina mama na
watoto katika hospitali hiyo kutokana.Vifo vya akina mama na watoto hapa
nchini bado ni vingi. Jitihada kubwa zinahitajika kuvipunguza. Kupitia
misaada ya wadau mbalimbali kama huu wa Benki ya KCB lengo linaweza
kufikiwa. Tunaishukuru sana Benki ya KCB kwa msaada huu muhimu.
Kwa
upande wake mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake hospitalini hapo Dr
Gileard Masenga alisema kuwa hospitali hiyo haikuwa na wodi ya akina
mama mahututi na kuongeza kuwa msaada huo utasadia kuokoa maisha ya
akina mama na watoto.
Mwanzoni
tulikuwa tunalazimika kuwapeleka akina mama kwenye hodi za wagonjwa
hahututi ambazo wagonjwa wote wanatibiwa. Tunaamini msaada huo utasaidia
kuboresha hali na hivyo kuokoa wakina mama wengi zaidi. Tunaishukuru
Benki ya KCB kwa kuwekeza katika afya ya mama na mtoto,” alifafanua
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)