amsha amsha ya tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya mji wa moshi leo. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

amsha amsha ya tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya mji wa moshi leo.

Sehemu ya  Wanaharakati wa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakiwa wamepozi mapema leo mchana mjini Moshi,mara baada ya kumaliza awamu yao ya kwanza ya kuruka hewani na amsha amsha ya tamasha hilo kwa wakazi wa mji wa Moshi,kutoka kulia pichani  ni Bonge,Eric Kusaga,Simon Malenga sambamba na Millard Ayote wote kutoka Clouds FM.Tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Moshi linatarajiwa kurindima ijumaa hii ndani ya Chuo cha Ushirika,ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni sh 5000 tu kwa kila mmoja,kama vile haitoshi kutakuwepo  na wasanii lukuki wa bongofleva akiwemo na aliyeshiriki shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezzoo.
Mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya kutoka Clouds FM akizungumza na mmoja wa mashabiki wa kituo hicho cha redio,mapema leo mtaa wa Ghala mjini Moshi,ikiwa ni sehemu ya mchakato mzima wa amsha amsha ya tamasha kubwa la Serengeti Fiesta,ambalo linatarajiwa kufanyika mjini humo siku ya ijumaa katika chuo cha ushirika.wasanii watakao shiriki kadhaa ni Joh Makini,Mwana FA,Linah,Godzilla,Juma Nature,Ommy Dimpoz,Bob Junior,Sheta,Ferooz,Richard Mavoko,washindi wa Supa Nyota na wengineo kibao.
Washkaji nao hawataki kupitwa kabisa na shughuli nzima ya mambo yanayoshushwa na Clouds FM,hapa walikuwa wakisikiliza kipindi cha amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lililokuwa likirushwa live hewani ndani ya mji wa Moshi mapema leo mtaa wa Ghala.
Kiongozi wa msafara wa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjini Moshi,Dj Mully B akiendelea kuweka mambo sawa kwenye gari yao ya matangazo ya live (OB-Van) kabla ya kuanza kuruka live,kati ni Eric Kusaga sambamba na Simon Malenga wakifuatilia kwa ukaribu kuhakikisha kila kitu kinakwenda.
Mmoja wa mashabiki damu wa Clouds FM akimuelekeza Millard Ayo shughuli zao mbalimbali wanazozifanya ikiwemo na namna wanavyoupanda mlima kilimanjaro wakiwa na wageni wao mbalimbali,hapa alikuwa akimuonesha sehemu ya Mlima Kilimanjaro uliokuwa uking'ara vizuri kabisa.
 Haa haaa ni wakati wa msimu si vibaya ukajivunia.
 Aaahh...jamaaani wewee ndio Millard Ayo..! yule anaetangaza kipindi cha Amlifaya Clouds FM..! wwooowww....! nafurahi kukuona,so how are u..!
Millard Ayo akiendelea na amsha amsha yake ya tamsha la Serengeti Fiesta kwa wadau mbalimbali mapema leo ndani ya mji wa Moshi,ambapo katika muendelezo wa tamasha hilo zimepangwa kutolewa zawadi kede kede,ikiwemo simu za mikononi,piki piki,fedha taslim na nyinginezo kibao,huku zawadi kubwa ikiwa ni ya gari aina ya Vits.
Kiongozi wa msafara wa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjini Moshi,Dj Mully B akitoa maelekezo mafupi namna ya kujishindia zawadi mbalimbali za Serengeti Fiesta kwa mdau wa Clouds FM.
Vijana mbalimbali waliojitokeza maeneo ya mtaa Ghala,jijini Moshi wakati wa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ambapo washabiki mbalimbali walijipatia fulana za Fiesta,tayari kwa kwenda kujiachia siku ya ijumaa ambapo tamasha hilo litakaporindima ndani ya chuo cha ushirika,ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni sh 5000 kwa kila mmoja,tamasha hilo baada ya kurindima mkoni Moshi pia litahamia mjini Tanga katika uwanja wa Mkwakwani siku ya jumapili.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages