ZOEZI LA KUENDELEA KUTAMBUA MAITI KATIKA AJALI YA MELI YA SKAGIT YAENDELEA HUKO ZANZIBAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ZOEZI LA KUENDELEA KUTAMBUA MAITI KATIKA AJALI YA MELI YA SKAGIT YAENDELEA HUKO ZANZIBAR

Wahusika wa Matayarisho ya Mazishi ya watu waliokuwa bado hawajatambuliwa na Jamaa zao ili kuzikwa kiserikali wakiwa katika kazi ya kutayarisha Sanda hapo katika Viwanja vya Maisara Zanzibar.
 Madaktari wakiandika Orodha ya Maiti zinazoletwa hapo katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar Baada ya kupatikana kutoka katika Meli ya Skagit iliozama hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar
 Baadhi ya Wananchi wakiwa wamekusanyika katika Viwanja vya Maisara ili kuweza kupata taarifa ya Ndugu zao waliokuwa katika Meli ya Skagit ambayo imepata Ajali ya Kuzama katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar
 Baadhi ya Wageni kutoka Nchi mbalimbali wakiwa katika Viwanja vya Maisara ili kujuwa Ndugu zao na kuangalia taratibu zinazofanyika viwanjani hapo kutokana na Kuzama kwa meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
 Wananchi mbalimbali wakizitambua Maiti zao zilizopatikana katika Ajali ya Meli ya skagit iliozama hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
 Baadhi ya Maiti za watoto zilizopatikana katika Ajali ya Meli ya Skagit iliozama zikiwa katika Eneo la Maisara kwa ajili ya kutambuliwa na Nduguzao.Hadi mchana huu Maiti zilizopatikana ni 39 kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Zanzibar na bado waokoaji wanaendelea na zoezi hilo katika eneo la Tukio.
 Baadhi ya wananchi wakiwa katika Foleni ili kwenda kuzitambua Maiti zao katika Viwanja vya Maisara kutokana na kuzama kwa Meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.Hadi mchana huu Maiti zilizopatikana ni 39 kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Zanzibar na bado waokoaji wanaendelea na zoezi hilo katika eneo la Tukio
 Baadhi ya Wananchi waliozitambua maiti zao katika Viwanja vya Maisara wakisaidiwa na Askari kutokana na Huzuni kubwa waliokuwanazo.kwa kuzama kwa Meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.Picha Na YUSUPH SIMAI - MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages