Baadhi
ya wanafunzi wa Darasa la saba wa Shule ya Msingi Lugalo ya Jijini Dar
es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wao, nje ya
Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma leo, wakati walipofika kutembelea na
kujifunza shughuli za Bunge, wakiwa katika ziara yao ya Kimasomo.
Wanafunzi hao wanatarajia kuondoka mjini Dodoma kesho Julai 4, kurejea
jijini Dar es Salaam, baada ya kumaliza ziara yao hiyo, ikiwa ni pamoja
na kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma.
Baadhi
ya wanafunzi wa Darasa la saba wa Shule ya Msingi Lugalo ya Jijini Dar
es Salaam, wakiwa kwenye Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, leo wakati
walipofika Bungeni hapo kwa ajili ya kutembelea na kujifunza shughuli za
Bunge wakiwa katika ziara yao ya Mkoa wa Dodoma inayomalizika leo
jioni.
Baadhi ya walimu wakipozi kwa picha na baadhi ya wanafunzi, nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
'Wabuge watarajiwa wa miaka ijayo', Baadhi ya wanafunzi wakipozi kwa picha nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
Miongoni
mwa wanafunzi hawa, wapo Walimu, Mawaziri, Makatibu, Madaktari, Wabunge
na Viongozi mbalimbali wa miaka ijayo, endapo watapewa misingi ya elimu
iliyo bora na kupewa elimu ya Nidhamu na utiifu wakiwa bado wadogo, ili
waje kuwa viongozi bora siku za baadaye.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)