Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa Yanga
uliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Julai 15 mwaka huu
ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Ushindi
waliopata wajumbe wapya sita waliochaguliwa kuingia kwenye Kamati ya
Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wanachama wa Yanga waliohudhuria
uchaguzi huo walivyo na imani kwao.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya Yanga
ambayo hivi sasa ina vinara wapya, na kwamba wana changamoto kubwa ya
kuhakikisha wanaendesha shughuli za klabu hiyo kwa kuzingatia katiba na
kanuni.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga chini ya Jaji Mkwawa na
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa
kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia katiba
na kanuni.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)