Mwananchi wa kijiji cha Mzuri Makunduchi Bakari Ubwa, akitoa maoni yake
mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ametaka kuwe na Serekali mbili
ya Zanzibar na Tanzania Bara na kila Serekali iwe na uwezo wake na Rais
wa Zanzibar awe na uwezo wa kuamua mambo yake kwa ajili ya Zanzibar,Rais
wa Zanzibar awe na uwezo wa kuchagua Mabalozi kwa ajili ya Zanzibar na
Rais wa Tanzania pia na yeye achaguwe mabalozi wa Tanzania.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Balozi Salim Ahmed Salim,
akizungumza kuhusiana na utoaji wa maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya
Tanzania katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Mtende.
Mwenyekiti wa Mkutano wa kutowa maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya
Tanzania Mohammed Yussuf Mshamba, akisoma vipengele wakati wa kutowa
maoni ya mabadiliko ya katiba katika viwanja vya Mtende Makunduchi.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania Dk Mvungi, akitowa
maelezo kwa Wananchi wa Kijiji cha Mtende waliofika kutoa maoni yao
katika viwanja vya Skuli ya Mtende.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania wakifuatilia maoni ya
Wananchi wa Kijiji cha Mzuri wakiyatowa mbele ya Tume hiyo ilioanza kazi
yake jana katika Wilaya ya Kusini Unguja Makunduchi Mkoa wa Kusini
Unguja.
Mwananchi wa Kijiji cha Mzuri Makunduchi akikabidhi barua yenye maoni
yake kuhusu Mabadiliko ya Katiba, mkutano huo umefanyika katika viwanja
vya mpira timu ya Mwenge Mzuri,
Mwananchi wa Kijiji cha Mtende Makunduchi Aziza Mcha, akikabidhi barua
yake yenye maoni yake kwa Mwenyekiti wa Mkutano wa kutowa maoni ya
mabadiliko ya Katiba ya Tanzania Mohammed Yussuf Mshamba, wakati tume
hiyo ilipofika katika Wilaya ya Kusini Unguja kukusanya maoni ya
Wananchi kuhusu Katiba, mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Skuli
ya Mtende.
Mwananchi wa Kijiji cha Mtende Ali Khamis Ali, akichangia maoni yake kwa
kuanza kwa historia kuhusu Mzee Karume, ambaye amesema Unguja itakuwa
kama peponi na kweli ilikuwa hivyo kwa kujenga Nyumba za Wazee Sebleni
na kuanzisha Viwanda mbalimbali katika Zanzibar.Amesema kuwepo kwa serikali mbili ya Zanzibar na Tanganyika na kutaka
kuwe na Muungano wa Mkataba na kugawana sawa kwa sawa misaada
inayopatikana. na mambo ya muungano kugaiwa sawa.
Mwananchi wa Kijiji cha Mzuri Makunduchi Duli Ali Duli, akichangia maoni
yake kwa Tume iliofika kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya
Katiba ya Tanzania, amesema kuwe na Serikali mbili ya Zanzibar na
Tanganyika, na kuondoa kasoro zilioko katika Muungano huu.
Mwananchi wa Mtende Abuu Kombo Ramadhani, ametowa maoni yake kuwe na
serekali mbili na kuwe na uwiano katika nafasi za Muungano kwa pande
mbili hizi na Zanzibar iwe na rasilimali zake wenyewe bila kuingiliwa na
upande mwengine. na bara iwe hivyohivyo.
Mwnchi wa Kijiji cha Mtende Mohammed Shaka Mussa, amesema nashukuru
kuitwa Tanzania na pia Umoja ni Nguvu,Utengano ni Udhaifu. Amesema
kuwepo na serikali mbili ya Zanzibar na Tanganyika na kila upande uwe na
uwezo wa kuamua mambo yake na kuondoa kasoro za Muungano zilizopo ili
kuimarisha umoja wetu.
Wananchi wa Kijiji cha Mzuri Makunduchi wakiwa katika viwanja vya
Mwenge wakishiriki kutowa maoni yao wakisikiliza maoni ya Wananchi
mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania.iliyofika katika kijiji
hicho kukusanya maoni ya Wananchi.
Wananchi wa Kijiji cha Mtende wakisikiliza maoni yanayotolewa na
Wananchi wa Mtende mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba katika viwanja
vya skuli ya Mtende
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania Balozi Salim Ahmed
Salim. akibadilishana mawazo na Wazee wa Kijiji cha Mzuri
Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja, baada ya kumalizika kwa utowaji wa
maoni kwa Wananchi wa Kijiji hicho.Picha Zote na Mdau Mapara Othman-Kusini Unguja
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)