NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
SERIKALI
imesema kuwa hakuna malipo ya kiasi kidogo cha fedha kilicholipwa kwa
waathirika wa mlipuko wa mabomu ya Kambi ya
jeshi ya Mbagala yaliyotokea mwaka 2009 kama ilivyoripotiwa na gazeti
moja la kila wiki la hapa nchini hivi karibuni.
Akizungumza
na Idara ya Habari( MAELEZO) jana ofisini kwake , Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Said Meck Sadick alisema hakuna fidia ya Shs. 1400 na Shs.
2500 iliyotolewa kuwa ni ya uharibifu wa jumla ya fidia za malipo kwa
wahanga hao, bali malipo hayo ni tofauti ya kiasi cha fedha
kilichokuwa kinadaiwa na wahanga hao ambacho kilichobakia.
‘’
Unajua malipo ya wahanga hao yalifanyika katika awamu mbili. Hivyo
kiasi cha fedha cha malipo hayo yaliyotolewa katika hundi hizo , ambayo
iliripotiwa katika gazeti hilo ni malipo ya awamu ya tatu. Malipo hayo
ni tofauti ya fedha kilichokuwa kinadaiwa na si kweli kuwa wahanga
hao walilipwa fedha hizo kama jumla ya fidia za malipo yao,’’ alifafanua
Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu
huyo wa Mkoa, aliongeza kuwa habari hiyo iliyoandikwa sio sahihi na
haikufuata maadili ya uandishi wa habari kwani hakuweka wazi usahihi wa
taarifa hiyo.Serikali haijamdhulumu mtu yeyote, bali inalipa kutokana
malipo stahili.
‘’Ninaomba
waandishi wa habari waandike habari walizozifanyika utafiti wa kina wa
pande zote ilikuepusha utoaji wa taarifa zisizosahihi,’’ alisisitiza.
Aidha
Mkuu huyo alisema malipo ya waathirika hao yanatolewa kwa awamu tofauti
na kwa idadi ya watu maalum, kwa sababu ya kuepusha utoaji wa malipo
yasiyostahili. Hivyo aliwataka waathirika hao kuvuta subira kwa
kuwa malipo hayo bado yanaendelea.
Naye
Mtathimini Mkuu wa malipo hayo, Victor Ndonne akizungumzia kuhusu
suala hilo alisema hundi za malipo ya sh. 1000 na zilizotajwa hapo juu
ni za tofauti ya kiasi cha fedha kilichobakia baada ya wahanga hao
kutoridhika na malipo hayo yaliyotolewa katika awamu ya kwanza na awamu
ya pili.
‘’
Fedha hizi zimelipwa baada ya kufanyika kwa tathimini mpya Agosti 18
mwaka 2011, ambapo ilioneka baadhi ya wahanga hawakurithika na fidia
walizolipwa,’’ alisema Ndonne .
Alifafanua
kuwa orodha ya wahanga wanaodaii malipa yao ni 2,575, hivyo hundi
zilizotolewa hadi sasa ni 295 kwa ajili ya malipo hayo, ambapo hundi 244
zimeshakabidhiwa kwa wananchi husika, hundi nyingine 18 majina
yamebandikwa katika eneo la Mbagala Kuu na Ofisi ya Mkurugenzi
wa Wilaya ya Temeke, zaidi ya wiki moja iliyopita na wanasubiri
wananchi waende kuchukua.
Ndonne
alisema hundi 32 zimeonekana kuwa na matatizo mbalimbali mfano majina
ya vitambulisho vyao ni tofauti na yaliyoandikwa katika hundi na majina
mengine ya hundi hizo wahusika wameshafariki dunia. Aidha aliongeza kuwa
hundi moja imeonekana majina yamejirudia.
Alisema
kuwa hundi za malipo ya fedha ya wahanga hao zilitolewa kabla ya
mwisho wa mwaka wa fedha uliopita. Malipo ya fedha zingine zitatolewa
mwaka huu wa fedha wa 2012/2013 mara baada ya Serikali kuidhinisha.
|
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)