■
Agombea mkanda wa Afrika wa IBF
akipeperusha bendera ya Tanzania nchini Namibia
Mtanzania
Rajabu Maoja bondia mzoefu katika ngumi za kulipwa kutoka mkoa wa Tanga atapanda
ulingoni Septemba 1 kupimana ubavu na bondia Gottlieb Ndokosho bingwa wa ngumi
nchini Namibia.
Mpambano
huo unaofanyika katika jiji na Windhoek, nchini Namibia unawakutanisha mabondia
wawili ambao wanazimudu vizuri ngumi ulingoni. Hii ni mara ya kwanza kwa bondia
wa Kitanzania kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika nje ya nchi tangu
mpambano katia ya Iraq Hudu na Ali Said wa Kenya ulivyofanyika jijini Mombasa
mwaka 2000.
Wawili
hao wataumana kwenye mpambano uliopewa jina la “The Battle for the Kalahari Desert” (Vita ya Jangwa la Kalahari) na
waandaaji wa mpambano huo ambao ni Kinda Boxing Promotion chini ya promota Simon
Nangolo wa nchi ya Namibia. Namibia iko Kusini Magharibi mwa bara la Afrika
ikikingana na Afrika ya Kusini, Botswana na Angola.
Mtanzania Rajabu maoja anatokea katika jiji la tanga na ni mkali aliyejijengea umaarufu mkubwa katika masumbi hapa nchini. Maoja ni kati ya mabondia wachache wenye majina yanayotishia maisha baadhi ya mabondia wenzake katuka bara la Afrika.
Katika
uhai wake wa ngumi Maoja amepigana mapambano 31 akishinda 18 na kupoteza kwa
kiduchu mapambano 10 ambayo mengi sio yenye hadhi yoyote ya kumharibia historia
yake kwemey ngumi na kutoka sare mapmbano matatu (3)
Naye
bondia Gottlieb Ndokosho ambaye ni bingwa wa Namibia amepigana pambano 15 na
kushinda 11 wakati amepoteza mapambano 3.
Mpambano
huo uliopewa jina la The Battle for the
Kalahari Desert (Vita ya jangwa la Kalahari) utasimamiwa na Rais wa
Shirikiso la ngumi la Kimataifa bara la Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya
Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Aidha Ngowi ndiye Rais w kamiehsni ya Ngumi za
Kulipwa nchini (TPBC) na mkurugenzi wa ngumi wa baraza la Ngumi la Jumuiya ya
madola.
Watanzania,
tumuezi mwenzetu Rajabu Maoja anapopeperusha bendera ya Tanzania. Mungu ibariki
Afrika, Mungu ibariki Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)