Ndege mpya ya Precision Air aina ya
Boeing 737-300 ikiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere tayari
kwa kufanya safari yake ya kwanza kuelekea Lusaka, Zambia kupitia Lubumbashi –
Congo DRC mapema leo.
Taswira ya ndani ya Boeing 737-300
iliyowasili wiki iliyopita toka Nairobi, Kenya ilipokuwa ikibadilishwa
muonekano wake kwa kupakwa rangi za Precision Air, pamoja na kuipatia kibali
cha kuruka katika anga za Tanzania na kimataifa pia.
Sehemu ya mkia wa ndege hiyo inayo
onyesha usajili wake nambari 5H-PKS. Precision Air pia ina ndege Boeing 737-300
mbili zingine zenye usajili 5H-PMS na 5H-PAZ. Kwa ujumla sasa shirika hilo la
ndege 12; ATR 72-500 tano, ATR 42 -500 mbili, ATR 42 -320 mbili na B737 -300
tatu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)