Mhe. Lowassa, Mama
Regina na Brigedia Jenerali Mabeyo wakikumbushana jambo.
Mweyekiti wa Kamati ya
Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowass ( Mb) na Waziri Mkuu Mstaafu
akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Brigedia Generali, Dkt.
Charles Muzanila kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) wakati wa kikao
cha majadiliano na kubadilishana mawazo kilichofanyika siku ya pili ya ziara ya
kikazi ya Ujumbe wa NUU. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makazi ya Balozi
yaliyoko eneo la Dobbs Ferry.
Mkutano wa
kubadilishana mawazo ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya NUU mara baada ya
wajumbe wa Kamati hiyo kutembelea na kukagua majengo yanayomilikiwa na
Serikali. Aliyesimama ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Esaka Mugasa,
akijibu na kutoa maelezo kuhusu hoja zilizoulizwa na Mwenyekiti, Mhe. Edward Lowassa.
Mwenyekiti akifurahia
jambo pamoja na wajumbe ambao hawapo pichani, kutoka kushoto ni Birigedia
Jenerali Venance Mabeyo, Kaibu Balozi Dkt Justin Seruhere, Mhe. Edward Lowassa
( Mb) na Mama Regina Lowassa.
" Nadhani hiki
kinamtosha Mzee" ndivyo anavyoelekea kusema Mama Regina Lowassa, wakati
akimsevia Mhe. Mwenyekiti mahanjumati yaliyoandaliwa na Ubalozi kwa heshima ya
wanakamati na wajumbe wanaohudhuria mikutano katika Umoja wa Mataifa. Maandazi
yalikuwapo na kachumbari ilikuwapo.
Mwenyekiti akiwa
katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati na wajumbe wengine wanaohudhuria
mkutano wa ATT na ECOSOC.
---
Na Mwandishi Maalum
Mwenyekiti wa Kamati
ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ( NUU) Mhe, Edward Lowassa(Mb) na Waziri
Mkuu Mstaafu, amewataka wajumbe wanaohudhuria mkutano wa majadiliano kuhusu
Mkataba wa Biashara ya Silaha ( ATT), kuhakikisha kwamba maslahi ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania yanazingatiwa.
Mhe. Lowassa ametoa
ushauri huo siku ya jumamosi wakati alipokutana na kubadilishana mawazo na
wajumbe wanaohudhuria mkutano huo wakiongozwa na Brigedia Generali, Dkt.
Charles Muzanila kutoka JWTZ.
“ Mkutano
unaendeleaje, na je kuna mwelekeo wowote” akahoji Mwenyekiti na kuongeza. “
Hakikisheni mnafuatilia kikamilifu majadiliano haya ili kuhakikisha maslahi ya
nchi yetu yanazingatiwa.
Mazungumzo kati ya
Ujumbe wa NUU wataalamu wanaohudhutia mkutano wa ATT yalifanyika katika makazi
ya Balozi wa Tanzania, yakihudhuriwa pia na wajumbe wengine wanaohudhuria
mkutano wa masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii ( ECOSOC) na Maafisa wa
Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa.
Wajumbe wa Kamati hiyo
unaowajumuisha wabunge watano akiwamo Mwenyekiti Mhe. Lowassa jana jumamosi
uliingia katika siku yake ya pili ya ziara yake ya Kikazi na Mafunzo hapa
Jijini New York, ambapo ni makazi ya Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tazania katika Umoja wa maraifa
Katika siku hiyo ya
pili wajumbe walianza siku yao kwa kupata taarifa ya masuala ya Utawala na
Fedha iliyotolewa na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi, Bw. Modest Mero akishirikiana
na Mshauri wa Masuala ya fedha wa Ubalozi Bw. Alfred Swere.
Baada ya kupokea
taarifa hiyo, wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Edward
Lowassa ( Mb), walitembelea , kukagua na kujionea hali halisi ya majengo
yanayomilikiwa na Serikali.
Majengo hayo ni lile
ambalo limenunuliwa na serikali na ambalo litatumika kama ofisi za Ubalozi wa
Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika UMoja wa Mataifa , jengo
ambalo baadhi ya ghorofa zake zitatumika kama kitega uchumi.
Kununuliwa kwa Jengo
hili lenye ghorofa sita na ambalo liko eneo la Manhattan sasa kunaifanya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na jengo la kudumu na lenye
hadhi ya Ubalozi.
Kwa miaka yote tangu
kufunguliwa kwa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, huduma
za Ubalozi huo zimekuwa zikifanyika katika ofisi za kupanga na hivyo kuigharimu
serikali gharama kubwa za kodi ya pango.
Kununuliwa kwa jengo
hili kutasaidia sana kupunguza gharama za kulipia pango lakini pia kuogeza
ufanisi na tija katika utendaji kazi na kulingizia pato taifa.
Baadaye ujumbe wa
Kamati hiyo ulitembelea jengo la pili ambalo ni mali ya serikali na makazi ya
Balozi wa Tanzania. Jengo hili liko eneo la Mt. Vernon lina historia ya aina
yake lakini kwa sasa halitumiki kama makazi ya Balozi kutokana na uchakavu na
hivyo kuhitaji matengenezo makubwa.
Baada ya kukagua na
kujionea hali halisi ya jengo hilo , wabunge walikwenda eneo la Dobbs Ferry
ambako ndipo yaliyo makazi ya muda ya Balozi.
Wakiwa katika makazi
hayo, Mwenyekiti wa NUU ujumbe wake, walipata chakula cha mchana
kilichoandaliwa na Ubalozi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)