Marehemu Agnes
B. King'unza wakati wa uhai wake.
Agnes alikuwa
ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa mwaka wa
kwanza akichukua Shahada ya Kodi (Bachelor of Taxation).
Mwili wa
marehemu Agnes ukiwa kwenye jeneza ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwao Mbezi kwa
Msuguri.
Mwili wa
Marehemu Agnes ukiwa kanisani tayari kwa heshima ya mwisho katika kanisa la
Romani katoliki Mbezi Temboni.
Mama Mzazi wa
Agnes akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa Mwanae.
Aliyevaa Koti
jeusi ndio baba mzazi wa Agnes Bwana Bernard King'unza.
Makamu Rais wa
Serikali ya wanafunzi wa IFM akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi
wenzake.
Baba Padre wa
Parokia ya Mbezi Temboni akibariki mwili wa Agnes King'unza.
Hawa ni baadhi
ya wanafunzi wenzake aliokuwa akisoma nao katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM
na kushoto mwenye shati la mistari ni mwakilishi kutoka wafanyakazi wa
IFM.
Agnes
aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni
mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu
wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa
hospitali ya Agha khan.
Marehemu
Agnes B. King'unza alifariki Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya
Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha
khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Mwili
wa Marehemu Agnes King'unza umesafirishwa jana Jioni kwenda Nyumbani kwao
Kalenga - Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika leo tarehe 19/07/2012.
BWANA
ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE













No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)