Kabonga Mohammed.
Tromøy, Arendal (Norway).
Mwanamke mwenye asili ya Tanzania anatafutwa, ametoweka nyumbani
baada ya kudai kudundwa na mumewe tangu Jumatatu .
Huyu
ndiye dada wa Kitanzania aliyepotea toka Jumatatu hajaonekana mpaka
leo. Bado anatafutwa! Polisi wanaomba msaada wa wananchi kwa yeyote
anayefahamu lolote kuhusu huyu dada.
Mbwa
wa polisi wakisaidia kwenye msako wa kumtafuta mwanamke mwenye asili
ya Tanzania aliyepotea Tromøy, Arendal. Picha na Anne Karin Andersen
(Agderposten)
Jana saa moja mwanamke mmoja alipiga simu polisi na kusema kuwa amepigwa nyumbani kwake. Baada
muda mfupi, akaonekana ametoka nyumbani kwake, maeneo ya Tromøy,
Arendal. Ametoweka na hajaonekana tokea jana. Mwanamke huyo ana asili ya
Tanzania.
Mumewe
alitoa taarifa polisi baada ya kutoonekana kwa muda mrefu. Tokea jana
amekuwa akitafutwa na helikopta, boti za polisi, polisi wenye mbwa,
jamaa wa msalaba mwekundu na watu wa kujitolea.
Source: http://watanzaniaoslo.blogspot.com/
Source: http://watanzaniaoslo.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)