Ujumbe
wa Tanzania ambazo kwa mwezi mzima umeshiriki kikamilifu hadi usiku
wa manane pale ilipobidi na kuhakikisha kwamba maslahi ya Tanzania
katika majadiliano ya kidiplomasia ya nchi wanachama kuhusu Mkataba wa
Kisheria wa Kudhibiti Bishaara ya Silaha duniani yalikuwa
yamezingatiwa. Hata hivyo mkutano huo ulioanza Julai Mbili na kumalizika
Julai 27 umeshindwa kutoa Mkataba kutokana na wajumbe kutokukubaliana
kuhusu baadhi ya vipengere ambavyo wengine walikuwa wanataka viwe sehemu
ya mkataba, huku wengine wakikataa kata kata.
Mkataba huo kama ungepatikana ulitarajiwa kwamba ungeleta matumaini na unafuu kwa mamilioni ya watu ambao maisha yao kila siku yamo hatarini kutokana na matumizi mabaya ya silaha. Inaelezwa kwamba biashara ya silaha duniani inashika nafasi ya pili baada ya biashara ya madawa ya binadamu. Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Bw. Theobald Kazora kutoka Ofisi ya Rais, Brigedia Jenerali Dkt. Charles Muzanila kutoka JWTZ ambaye pia alikuwa kiongozi wa ujumbe, Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere ambaye pia alikuwa kiongozi wa ujumbe akisaidia na Brigedia Jenerali Muzanila na Bw. John Kinuno ambaye ni wakili kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kutoka kulia mstari wa nyuma ni Bw. Peter Macomara kutoka Taasisi ya Kiraia, Brigedia Jenerali Venance Mabeyo kutoka JWTZ na Kamishna Esaka Mugasa kutoka Jeshi la Polisi na Mwambata Jeshi katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Meja Wilbert Ibuge ambaye hayupo pichani.
Na Mwandishi Maalum
Matarajio
na matumaini ya kupatikana Mkataba wa Kisheria wa Kudhibiti Biashara
ya Silaha Duniani ( ATT) yameishia ukiongoni baada ya nchi wanachama
kushindwa kuzikabili tofauti za kimsimamo na kimaslahi.
Kuanzia
tarehe Mbili hadi 27 mwezi huu wa Julai , wajumbe kutoka mataifa
karibu yote duniani ikiwamo Palestina na Holly Sea, na Vyama Kiraia
walikutana hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwa lengo moja kuu na
muhimu sana, mstakabali wa biashara ya silaha duniani.
Pamoja
na kujadiliana , wakati mwingine hadi usiku wa manane kuhusu umuhimu na
malengo ya kuwa na Mkataba huo, nchi hizo hazikuweza kukubaliana kuwa
na mkataba ambao ungesimamia ununuzi na matumizi ya silaha za aina
mbalimbali zikiwamo pia risasi.
Kutofikiwa
kwa Mkataba huo licha ya kutolewa kwa rasimu ambayo ilijitahidi
kukidhi matarajio na maslahi ya kila nchi kumetokana na kutokukubaliana
kwa vipengele vichache ambavyo baadhi ya nchi zilitaka viingizwe.
Vipengele
ambayo vilishindikana kupatiwa ufumbuzi hadi siku ya mwisho ya
majadiliano ni pamoja na, Baadhi ya Nchi zinazouza na kuzalisha silaha
kutokuwa tayari kuingiza kwenye mkataba huo risasi na mabomu, huku nchi
nyingine zikisisitiza vipengere hivyo viingizwe na kuwa sehemu ya
mkataba.
Aidha
nchi zilishindwa kukubaliana pendekezo lililokuwa limetolewa na mataifa
ya Kiarabu la kutaka suala la Palestina la kujiamulia mambo yake
liingizwe kwenye mkataba. Pendekezo hilo lilipingwa vikali na nchi za
Ulaya na Marekani.
Vipengele
vingine ambavyo vimechangia kutopatikana kwa Mkataba huo, ni kuhusu
pendekezo la kutaka Taasisi na Mashirika ya Kikanda yanayo jihusisha na
kuangalia matumizi ya silaha kutaka yapewe nafasi katika Mkataba huku
baadhi ya nchi zikipinga pendekezo hilo.
Halikadharika,
suala la Haki za kijinsia lilichagizwa na baadhi ya nchi likitaka
liingizwe kwa kisingizo kwamba matumizi holela ya silaha yamekuwa ya
kisababisha matatizo makubwa. Baadhi ya nchi hususani za Afrika
zilipinga kuingizwa kwa kipengele hicho zikitumia kigezo kwamba hadi
sasa hakujawa na tafsiri sahihi ya neno usawa wa kijinsia kutoka na
baadhi ya mataifa ya magharibi kulazimisha kutambua haki za mashoga.
Kipengere
kingine kilihusu kuingizwa kwa risasi kwenye mkataba, jambo lilozua
mvutano na mabishano makali, huku nchi kubuwa zikikataa kata kata
kuingizwa kwa risasi kwenye mkataba huku zikitishia kwamba zisingekuwa
tayari kusaini mkataba huo kama risasi zingeingizwa.wapo
“Ninasikitika
sana kwamba tumefika hapa tulipofika, hayakuwa matarajio yangu mimi
kama rais wa mkutano huu na wala hayakuiwa matarajio yenu. Yalikuwa ni
majadiliano magumu, yaliyojaa hisia kali tulijitahidi tulivyoweza
kujaribu kuweka sawa maslahi ya kila upande. Lakini tumeshindwa kutoka
na Mkataba” akatamka Balozi Roberto Garcia Morita wa Argentina
aliyekuwa Rais wa Mkutano huo.
Akiongea
kwa masikitoka makubwa Balozi Roberto Morita amesema kukata tamaa.
“ Sitaki kusema mengi nisije nikatafsiriwa vibaya, ninaomba nibebe
dhamana hii ya kushindwa kufikia malengo ya kuwa na mkataba.
Nawashukuruni nyote kwa hatua hii tuliyofikia ingawa tumeshindwa kukidhi
hamu na matarajio ya watu”.
Ingawa
majadiliano kuhusu kuanzishwa kwa mkataba wa kudhibiti biashara ya
silaha yalikuwa magumu na ingawa mkataba huo haukupatikana. Lakini
majadiliano hayo yaliwezesha kupatikana kwa Rasimu ambayo kama
isingekuwa kwa vipengele vilivyotajwa hapo juu kuzua mvutano katika siku
za mwisho basi Mkataba ungepatikana. hatimaye chini ya usimamizi wa
raisi wa mkutano huo.
Karibu
nchi zote ambazo zilipata nafasi ya kuzungumza baada ya Rais kutamka
kuhitimisha kwa mkutano huo, ziliongea kwa hisia na kuelezea namna gani
zilivyosikitishwa na matokeo hasi ya mkutano huo. Lakini zikaahidi
kwamba zitakuwa tayari kuendelea na majadiliano hapo baadaye na hasa kwa
vile sasa wanatambuana vilivyo na wanajua misimamo ya kila nchi.
Baadhi
ya nchi kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mjumbe wake aliezea
kwamba kushindwa kupatikana kwa mkataba huo ni kielelezo cha wazi
kwamba wananchi wa DRC ambao hawajawaji kuonja amani na usalama kwa
miaka mingi wataendelea kuathirika.
“
Sote tunajua kwa nini tumefika hapa, silaha ni biashara ya pili kwa
ukubwa baada ya ile ya madawa. Ni kweli tunasikitika kwa matokeo haya
lakini hatujakata tamaa, tutaendelea kujadiliana ili hatimaye tuje kuwa
na mkataba wa kudhibiti silaha. katika siku za baadaye tuje kuwa na
mkataba.
Mkataba
huo wa Kisheria kwa Kudhibiti Biashara ya Silaha Duniani kama
ungepatikana basi silaha ambazo zingeguswa na mkataba ni pamoja na
Magari ya Deraya, Helkopta za kivita, ndege za kivita, vifaru, magari ya
kubeba mizinga, makombora, silaha ndogo na nyepesi.
Aidha
mkataba huo pia ungedhibiti suala zima la ununuzi wa silaha hizo,
usambazaji ,matumizi yake na kuhakikisha kwamba haziangukii mikononi
mwa wahalifu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)