Baadhi
ya wanafunzi wa shule za Msingi za jijini Dar es Salaam, Morogoro na
Singida, wakiandamana leo asubuhi kupinga hatua ya walimu kugoma kuingia
madarasani kufundisha jambo ambalo wanafunzi hao wamelielezea kuwa ni
kunyimwa haki zaoza msingi kuwakosesha masomo, ambapo nao wamepanga
kutinga Mahakamani kuwafungulia kesi walimu wao kutokana na kwamba madai
wanayoidai Serikali wao hayawahusu na hawahusiki kwa mamna yeyote ile,
alisikika mmoja wa viongozi wa wanafunzi hao aliyejitambulisha kwa jina
la Shaban Mudunda.
DAR:-
Wananfunzi wa Shule ya Msingi Mbezi ya Jijini Dar es Salaam, nao
hawakuwa nyuma katika kudai haki yao ambapo nao walifikisha ujumbe kwa
njia hii ya Bango, wakiwa pembezoni mwa barabara Morogoro leo asubuhi.
Nako
Mkoani Singida wanafunzi walijitokeza kwa wingi katika mitaa ya mji huo
huku wakiimba na wakiwa na baadhi ya Mabango yenye ujumbe kuhusu tukio
hilo la kugoma kwa walimu.
Hawa ni Wanafunzi
wa shule za msingi za Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani ktk
Manispaa Singida, wakiwa nje ya Ofisi za Mkuu wa mkoa huo leo asubuhi,
ili kumfikishia ujumbe baada ya walimu wao kugoma.
Wakati
walimu wakigoma kuingia madarasani leo asubuhi na wanafunzi wengine
kushika mabango na kuandama ili kufikisha ujumbe wa kudai hazi zao,
ilikuwa ni tofauti kwa wanafunzi hawa wa Shule ya Msingi Yeta, ambao wao
waliamua kuwaonyesha walimu wao kuwa hata wao wanaweza ambao wanafunzi
wa Darasa la Saba waliamua kujitolea na kutinga madarasa ya chini na
kushusha Nondoz kwa wadogo zao.
Na
katika Shule ya Msingi Lugalo, leo baada ya walimu kugoma wanafunzi wa
shule hiyo, walifundishwa na Ma MP pamoja na wanafunzi wa Darasa la saba
walifanya kama ambavyo wamefanya wanafunzi wa Yeta amapo wao pia
wamejitolea kuwafundisha wadogo zao wa madarasa ya chini.
********************************************
Na: Elisante John Singida.
MGOMO
Uliondaliwa Chama cha walimu CWT nchini, umeleta madhara katika
Manispaa Singida, baada ya wanafunzi wa shule za msingi kuandamana hadi
ofisi za Mkuu wa Mkoa leo asubuhi.
Kwenye
maandamano hayo, watoto wa shule za msingi Nyerere, Singidani, Ipembe
na Unyankindi, waliamua kutembea umbali wa kilomita tatu hadi ofisi za
Mkuu wa Mkoa, wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali huku barabarani
wakiimba '‘tunataka haki zetu, walimu wamegoma, tunataka haki zetu'’.
Baada
ya askari polisi kubaini usalama wa watoto hao upo hatarini,
waliingilia kati na kuongoza maandamano hayo hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa
kwa amani.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)