ELCT/KARAGWE DIOCESE
Kwa wadau wote wa
Maendeleo
Mkoa wa Kagera
Yah: MAOMBI YA MCHANGO KUFANIKISHA
MALENGO YA SHEREHE YA MIAKA 100 YA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA
KARAGWE
- NYAKAHANGA DDH
Somo hapo juu linahusika.
Hospitali tajwa inaadhimisha
miaka 100 tangu kuanza kutoa huduma za tiba na afya katika wilaya ya Karagwe. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni: Shabaha
Yetu ni Huduma Bora za Afya na Tiba
Maadhimisho hayo yatafanyika
tangu tarehe 27 Agosti na kilele kuwa tarehe 2 Septemba. Katika wiki hii, kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali
kutakuwa na maonyesho yatakayoenda sambamba na utoaji wa huduma za afya
bure kwa wananchi watakotembelea mabanda yaliyoandaliwa.
Uchunguzi wa afya kama vile
Kisukari, moyo, shinikizo la damu, upimaji wa VVU, uchunguzi wa saratani ya
matiti kwa akina mama, huduma za macho na uzazi n.k zitatolewa kwa kushirikiana
na wataalam wa ndani na nje ya nchi.
Mbali na huduma hizo, malengo
makubwa ya hospitali katika kuadhimisha miaka 100, ni kupambana na changamoto
zilizopo wilayani na nchini kwa ujumla katika kutoa huduma bora za afya.
Baadhi ya changamoto hizo ni
upungufu wa wataala wa kada mbalimbali na uchakavu wa miundo mbinu.
Kupitia sherehe hizi, hospitali
ina mpango wa kuanzisha chuo cha taaluma za afya na tiba wilayani Karagwe mapema
mwakani.
Chuo hicho kitatoa wataalam
katika fani za Uuuguzi, Uganga, wataalam wa Maabara na Maafisa afya.
Ø
Faida za Chuo hiki:
o
Kusaidia kupunguza upungufu wa wataalam Mkoani Kagera na nchini kwa ujumla.
o
Kusaidia vijana wanaomaliza elimu ya sekondari kupata elimu
ya taaluma kwa gharama nafuu, zingatia mkoa hauna chuo cha waganga, ni gharama
kubwa kwa wazazi kupeleka watoto wao nje ya mkoa kusomea taaluma hio.
o
Chuo kitatoa nafasi nzuri kwa watumishi waliopo kazini
kuweza kujiendeleza wakingali katika mazingira ya familia zao hivo kupunguza
gharama na usumbufu wa kusomea nje.
o
Chuo kitasaidia kuongeza ajira hivo kusaidia katika ukuaji
wa uchumi wa mtu mmoja mmoja, familia na taifa kwa ujumla.
Katika kufanikisha malengo
hayo, jumla ya shilingi 1.8 billion zinahitajika. Ikiwa ni kwa ajili ya
uendeshaji wa maadhimisho (utoaji wa huduma bure kwa wiki ya maadhimisho),
ukarabati wa miundombinu na ujenzi wa chuo.
Kwa niaba ya menejiment ya
hospitali, nakuomba ewe mpenda maendeleo uchangie kufanikisha malengo haya kwa
maendeleo ya sekta ya afya.
Wote watakao changia
wataorodheshwa katika kitabu maalum cha kumbukumbu.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu
kwa Mganga Mkuu: 0762 751 335 / 0712 916 800
/ 0787 785 969
Shukrani
Dr. Andrew
Cesari
Mganga
Mkuu
Nyakahanga
Hospital
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)