Meneja
masoko wa Kinywaji cha Grandmalt Fimbo Buttalah Kulia akimkabidhi
makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif
Ally Iddy Fedha Shilingi milioni tano kama sehemu ya Rambirambi
zilizotolewa kwa pamoja kati ya Grandmalt ambao ni wadhamini wa Ligi kuu
ya Zanzibar na Chama cha Soko Zanzibar ZFA. Kushoto ni Makau wa rais wa
Zfa Kassum Suleman
Meneja
masoko wa Kinywaji cha Grandmalt Fimbo Buttalah Kulia akimkabidhi
makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif
Ally Iddy Hundi ya Shilingi milioni tano kama sehemu ya Rambirambi
zilizotolewa kwa pamoja kati ya Grandmalt ambao ni wadhamini wa Ligi kuu
ya Zanzibar na Chama cha Soko Zanzibar ZFA. Kushoto ni Makau wa rais wa
Zfa Kassum Suleman
Makamu
wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally
Iddy akizungumza katika hafla fupi ofisini kwake wakatiti akipokea fedha
taslimu shilingi milioni tano toka Grandmalt na ZFA Kwaajili ya
kuwafariji wale wote waliopatwa na maafa ya ajali ya meli hivi karibuni.Picha zote kwa hisani ya Intellectuals Communications Limited
----
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
WADHAMINI
wa Ligi Kuu ya Zanzibar, ambao ni kinywaji kisicho na kilevi cha Grand
Malt kwa kushirikiana na chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA),
wametoa mkono wa pole kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ikiwa
ni kiasi cha Sh milioni 5, kwa ajili ya waathirika wa ajali ya boti ya
MV Skagit, iliyotokea hivi karibuni.
Akikabidhi pole hiyo kwa Makamu wa Pili wa SMZ, Balozi Seif Idd, Meneja
Masoko
wa Grand Malt, Fimbo Butallah alisema wameguswa na tukio hilo na
wameamua kuungana na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu.
“Tumeguswa
na tukio hili na kama Grand Malt ambao tuko hapa Zanzibar kama
wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya hapa, tumeamua kuungana nanyi katika
kipindi hiki.
“Tunapenda
kuwapa pole wote waliofiwa na wale wote waliokuwemo katika boti hiyo na
kwa ujumla kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Watanzania wote kwa
ujumla,” alisema.
Meneja
wa Grand Malt, Consolata Adam naye alisema walishitushwa baada ya
kupata taarifa ya ajali hiyo na kuamua kuungana na wengine katika kutoa
pole yao.
Makamu
wa rais wa chama cha mpira wa miguu zanzibar (ZFA)Ally Mohamed, Kassim
Suleiman naye alisema walishitushwa pia na ajali hiyo, kwani wamepoteza
watu ambao walikuwa mhimili mkubwa katika maendeleo ya mchezo huo
visiwani.
Balozi
Idd, aliwashukuru Grand Malt kwa pole yao na kusema atafikisha salamu
zao kwa wahusika na kuitaka pia iendelee kuwa na moyo huo wa kusaidia
pia michezo ndani ya Zanzibar.
Ajali ya MV Skagit ilitokea hivi karibuni katika eneo la Chumbe, Zanzibar na kupoteza maisha ya Watanzania kadhaa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)