Meneja
Mauzo wa Zantel mkoani Mbeya, Agrey Mwakilema nimiongoni mwa watu
kibao waliojitokeza kuchangia damu, zoezi ambalo limepokelewa vyema na
vijana waliojitokeza katika usaili huo siku ya kwanza hapa Club Vybes.
Majaji
sasa waliingia kazini na hapa wapo makini kumsikiliza mmoja wa
washiriki katika usaili huo. Kutoka kushoto ni Master J, Madam Ritha na
Salama Jabir. Kazi ilikuwa ngumu maana zaidi ya vijana 600 leo tu
walijitokeza sijui kesho itakuaje.
Vijana wakiwa nje wakisubiri kuingia katika mchujo.
Huyu
kwa leo amevunja rekodi ya Mkoa wa Mbeya ni mshiriki mdogo kuliko wote
aliyeingia katika usaili kutoMbeya na anaenda kwa jina la GOODLUCK BROWN. Akina Dogo Janja kibao mwaka huu huenda wakapatikana kama hawa wa Mbeya
Majaji
wa EPIQ BSS wakiwa wamesimama kimya kwa dakika mbili ili kutoa heshima
kwa watu waliopoteza maisha katika ajali ya Boti ya MV Skagit iliyozama
juzi huko Zanzibar kabla ya kuazan kwa usaili wa vijana watakao shiriki
shindano hilo kutoka Mkoani Mbeya ambapo zoezi linafanyika kwa siku
mbili Julai 21-22, 2012 katika ukumbi wa CLUB VYBES mjini Mbeya. Majaji
hao kutoka kushoto ni Salama Jabir, Madam Ritha, Masta J na Meneja
Mawasilino wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Awaichi Mawala.
Vijana
kibao wa mjini Mbeya wamejitokeza kuwania nafasi ya kuwakilisha mkoa
huo katika shindano la EPIQ BSS mjini Mbeya na hapa ni vijana waliofika
Club Vybes katika usaili wakibandika namba zao.
Baadhi
ya washiriki waliojitokeza katika usaili huo wakiwasikiliza maelekezo
kutoka kwa wasimamizi kabla ya kwenda mbele ya majaji.
Vijana
wakijipanga mistari kwenda kupokea namba na huku wengine wakiondoka
baada ya kupata namba zao na wanasubiri kwenda kushuka mistari yao kwa
majaji.Picha Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)