Mabondia, Francis Cheka (kushoto) na
Japhert Kaseba, wakitunishiana
misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao unaotarajia kufanyika Siku
ya tarehe saba mwezi wa saba katika uwanja mpya wa taifa ambapo kutakuwa
na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii nchini wakiongozwa na
Diamond pia kutakua na mechi ya Bongo Move na wasanii wa Bongo Fleva
watakapochuana kwa mara nyingine katika mpambano uho ulioandaliwa na
Global na kuratibiwa na Kaike Siraju utakuwa ni mpambano wa kwanza wa
Masumbwi kufanyika katika uwanja mpya wa Taifa
Baadhi ya mabondia watakaosindikiza mpamnbano huo ni Adiphoce Mchumia tumo atakaedundana na Ramadhani Kido wakati Amos Mwamakula ataoneshana kazi na Rashini Ali uku Mkongo Kanda Kabongo akizipiga na Said Mbelwa wakati bondia chipkizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala inayonolewa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli Masta na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'Super D' watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba
Baadhi ya mabondia watakaosindikiza mpamnbano huo ni Adiphoce Mchumia tumo atakaedundana na Ramadhani Kido wakati Amos Mwamakula ataoneshana kazi na Rashini Ali uku Mkongo Kanda Kabongo akizipiga na Said Mbelwa wakati bondia chipkizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala inayonolewa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli Masta na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'Super D' watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana mbalimbali
DVD YA FLOYD MAYWEATHE MPAMBANO WAKE WA MWISHO KABLA YA KWENDA JELA
NAYO INAPATIKANA KWA MAELEZO ZAIDI PIGA NAMBA 0713 406938,0787
406938,0754 406938 NA 0774 406938 AU FIKA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU
NA MSIMBAZI ULIZA SUPER D AU FIKA KLABU YA ASHANTI ILALA AU AMANA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)