Alumni wa Mlimani Primary wakishusha vitendea kazi.
Shule ya Msingi Mlimani ni moja kati ya shule kongwe
hapa Tanzania. Shule hii ilianzishwa miaka ya sitini na hadi sasa imetoa
vijana wengi wanaolitumikia Taifa la Tanzania kwenye Nyanja mbalimbali.
Shule hii iliyopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Vijana wengi
wa Chuo Kikuu, Savei, Makongo, Sinza, Kimara na maeneo ya karibu
wamepita hapo Kutokana na kula chumvi nyingi, majengo na miundo
mbinu ya shule hii iamechoka. Ili kuboresha majengo vijana waliosoma
hapo wakajikusanya na kuanzisha ‘’ Giving Back to Mlimani Day’’.
Mwaka huu siku hii iliangukia jumamosi ya Tarehe 30 June 2010. Alumni
wa Mlimani wanawashukuru mno wadau waliotoa; Jasho, Fedha , Muda na
kusaidia kufanikisha shughuli hii.
Moja ya madarasa yaliyofaidika na ‘’Giving back
to Mlimani’’
Alumni wa Mlimani wakiwa kwenye picha na Mwalimu Msuya kwenye ‘’Giving back to Mlimani’’ |
Kazi na dawa, misosi pia ilikuwepo; Huila, Victor
matondane na wadau wengine wakipata menu.
Dr. Tage akipaka rangi huku Salma Magimbi akimpa muongozo
Mdau wa Mlimani primary Imani Kajula akipiga ‘’chepe’’
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)