Kutoka Kushoto: Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa, Mkuu wa
Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya wakipokea msaada wa sehemu ya tani 200
za mahindi kutoka kwa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,
Dennis Hoof (wa pili kulia)na Makamu wa Rais wa African Barrick Gold
(ABG),Utekelezaji Muundo, Peter Gereta katika hafla iliyofanyika katika
Kata ya bulyanhulu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga hivi karibuni.
Maeneo yatakayonufaika na msaada huo uliogharimu kiasi cha milioni 163/-
ni kwa wale waliokumbwa na uhaba wa chakula katika vijiji 14 vilivyoko
Bugarama, Mwingiro na Bulyanhulu wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga na
Nyang'hwale Mkoa mpya wa Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya akipokea msaada wa tani 200 za
mahindi kutoka kwa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis
Hoof (wa pili kulia). Kushoto ni Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, Joseph
Makoba.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa akihutubia kabla ya makabidhiano.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya akihutubia kabla ya
makabidhiano. Kulia ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,
Dennis Hoof na Kushoto ni Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, Joseph Makoba
na Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa.
Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu wa
Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof (katikati), na Makamu wa
Rais wa African Barrick Gold (ABG),Utekelezaji Muundo, Peter Gereta.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya.
Kutoka Kushoto: Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis
Hoof , Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya na Mkuu wa Wilaya ya
Nyang'hwale, Ibrahim Marwa wakikagua sehemu ya shehena ya mahindi mara
baada ya makabidhiano.
Sehemu ya viongozi wa vijiji lengwa na msaada huo waliohudhuria hafla hiyo.Picha Zote na Badi John
Cha kushangaza ni kwamba mkoa unaopewa msaada ni mkoa unaoongoza kwa uzalishaji wa madini ya Almasi na Dhahabu Tanzania. Pia unaongoza kwa kuwa na wafugaji wengi zaidi wa Ng'ombe katika nchi yetu. Kama hiyo haitoshi, mkoa huu ni katika mikoa inayolima Mahindi, Mpunga, Mihogo na viazi kwa wingi ndani ya Tanzania yetu. Ni lini tutaacha kuingiza mambo ya siasa katika kila jambo tunalofanya? Ukiangalia picha hapo hao wanasiasa wanaona wamefanya jambo la kishujaa sana katika kupokea msaada. Wananchi either hawatambui nini kinaendelea au wanawaona jamaa wamewaona majuha kupitiliza. Tuache siasa nyingi!!!
ReplyDelete