Afisa
uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kushoto) akimkabithi bw. Bernard
Chezue modem baada ya kuibuka kuwa mshindi wa droo ya kila siku
inayowawezesha wateja wa Airtel waliofanya malipo ya bidhaa katika
viwanja vya sabasaba kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kila siku.
Akishuhudia ni mfanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel bi. Monica
Mgalwa.
Mshindi
wa droo ya kila siku ya Airtel money bwana Frank Joakim Mgumba
akijaribu kutumia simu yake mara baada ya kuibuka kuwa mshindi katika
droo inayohusisha wateja wa Airtel walionunua bidhaa kwa kupitia Airtel
money katika maonyesho ya Sabasaba. Pichani Katikati ni Afisa
uhusiano wa Airtel Jane Matinde pamoja na wafanyakazi wa Airtel huduma
kwa wateja wa viwanja vya sabasaba.
Mfanyakazi
wa huduma kwa wateja wa Airtel bi Monica Mgalwa akichezesha droo ya
kuchagua mshindi wakati wa kuchezesha droo ya kila siku iliyofanyika
jana katika viwanja vya sabasaba ambapo wateja watano walionunua bidhaa
kwa kupitia huduma ya Airtel money walijishindia zawadi mbalimbali
ikiwemo simu, modem na muda wa maongezi.Wakishuhudia pichani ni
wafanyakazi wa Airtel
Afisa
uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kushoto) akimkabithi mshindi wa droo
ya kila siku Bw Rucha Selemani modem baada ya kuibuka kuwa moja kati ya
washindi wa siku , droo hiyo inahusisha wateja waliofanya malipo ya
bidhaa kupitia Airtel money katika viwanja vya Sabasaba kuweza
kujishindia zawadi mbalimbali kila siku. Akishuhudia ni mfanyakazi wa
huduma kwa wateja wa Airtel bi Heleni Kimati.
Wanafunzi
wa shule ya msingi ya Neema Academy iliko jiji Dar es salaam wakipata
maelekezo kuhusu huduma ya internet ya 3.75G kutoka kwa mfanyakazi wa
kitengo cha huduma kwa wateja baada ya kutembelea banda la Airtel
lililopo katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba.
Wanafunzi
wa shule ya msingi ya Neema Academy iliyopo jijini Dar es salaam
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea banda la Airtel
lililoko katika maonyesho ya Sabasaba kilwa Road Dar es Saalam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)