Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Mwenyekiti wao Jacob Steven "JB"
wakiwa kwenye picha ya pamoja na Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa
ya Bombo jijini Tanga.Wasanii hawa wametembelea Hospitali ya Bombo
mapela leo asubuhi kwa ajili ya kukabidhi msaada wa Vyandarua katika
hospitali hiyo,ikiwa ni sehemu ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria
unaopoteza maisha ya watanzania wengi katika maeneo mbali mbali ya
nchini.Msaada huo umekabidhiwwa hospitalini hapo kwa hishani ya kampuni
ya Bia Tanzania Kupitia kinywaji Chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini
wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa
leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa wamezunguka kitanda cha Mmoja wa Mama
aliejifungua watoto Mapacha katika Wodi ya Wazazi wa Hospitali ya Bombo
Jijini Tanga mapema leo asubuhi wakati walipofika kutoa Msaada wa
Vyandarua kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Kinywaji chake
cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za
Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya
Tangamano Jijini Tanga
Msanii wa Bongo Movie,Mayassa Mrisho akikabidhi Chandarua kwa Mama
aliejifungua watoto mapacha kwenye hospitali ya Bombo,Tanga mapema leo
asubuhi.Picha na Othman Michuzi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)