WAKUFUNZI WA SENSA WAPIGWA MSASA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

WAKUFUNZI WA SENSA WAPIGWA MSASA

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi  ya Taifa ya Takwimu Dkt  Albina Chuwa akitoa ufafanuzi kwa wakufunzi wa Sensa  kwa ngazi ya kitaifa jana mjini Dodoma. Wakufunzi  hao wanaandaliwa kwa ajili ya kwenda katika mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwaelimisha wengi watakaosaidia kufanikisha zoezi la sensa tarehe 26 mwezi Agosti mwaka huu.
Baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakiwa watulia kimya kwa dakika mbili kwa ajili ya kuombeleza kifo cha Mhariri wa Jamboleo Willy Edward kilichotokea mjini Morogoro alipokuwa akihudhuria mafunzo ya sense kwa wahariri . Viongozi na wakufunzi hao walikuwa katika mafunzo  ya siku 10 tayari kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za mikoa . Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)yalianza jana mjini Dodoma.
Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho akitoa neno la utangulizi kwa  wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakati wa  mafunzo  ya siku 10 tayari kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za mikoa . Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) yalianza jana mjini Dodoma.
Baadhi ya wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakiwa katika mafunzo  ya siku 10 tayari kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za mikoa wakifuatilia mafunzo kutoka kwa wataalam mbalimbali walikuwa wakitoa mada mbalimbali. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) yalianza  jana mjini Dodoma.PICHA NA VICENT TIGANYA WA MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages