TASWIRA ZA KHADIJA KOPA NA MWANAHAWA ALLY WALIVYOPELEKESHANA PUTA DARLIVE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TASWIRA ZA KHADIJA KOPA NA MWANAHAWA ALLY WALIVYOPELEKESHANA PUTA DARLIVE

 Zuhura Shaaban wa Melody akiimba.
Mashabiki wa bnuruidani waliofika katika ukumbi wa Dar LIVE, Mbagala jana walipata  burudani ya nguvu kutoka kwa magwiji wa taarab nchini – Khadija Kopa, malkia wa kundi la TOT, na malkia wa kundi la Melody, Mwanahawa Ally. Burudani hiyo ilisindikizwa na bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa.
  Mwanahawa Ally akiimba wimbo wa ‘Kinyago cha Mpapure’.
 Wanamuziki wa bendi ya Mashujaa, Gado ‘Field Force’ (kushoto) akiimba na Chalz Baba.
 Abdul Misambano wa TOT akiimba.
 Chalz Baba akiwapa raha mashabiki.
  Wanamuziki wa TOT wakiitikia ‘mashairi’ ya Khadija Kopa.
  Wanenguaji wa bendi ya Mashujaa wakiwajibika.
 Mkurugenzi wa ukumbi wa Equator, Hamis Slim, akimtunza Khadija Kopa.
  Rapa wa Mashujaa, Ferguson, akighani na kunengua na mpiga gitaa wa bendi hiyo.
 Mwanamuziki wa Mashujaa, Gado, akitoa burudani.
 Khadija Kopa akiwa na mumewe kabla ya kupanda jukwaani kutoa burudani.
 
 Mashabiki waliofurika ukumbini humo wakijimwayamwaya na burudani.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages