Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua shamba la nyanya na mazao
mengine ya mboga pamoja na mizabibu katika shamba linalomilikiwa na
kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade, lililopo kijiji cha Chikopelo,wilaya
ya Bahi, Mkoani Dodoma leo asubuhi. Kushoto ni mmoja wa wamiliki wa
Shamba hilo Bwana Alon Hoven, anayeshirikiana na Bwana Dunstan Mrutu
(hayupo pichani). Shamba hilo linamwagiliwa kwa kutumia teknolojia ya
matone (Drip irrigation system).
Mmoja
wa Wamiliki wa Shamba la Mboga katika kijiji cha Chikopelo Bwana Alon
Hoven, kimwonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, baadhi ya mazao
yanayozalishwa kwa kutumia mbegu bora pamoja na teknolojia ya ya
umwagiliaji wa matone wakati Rais alipotembelea shamba hilo katika
kijiji cha Chikopelo, wilayani Bahi,mkoani Dodoma leo asubuhi.Shamba
hilo lenye ukubwa wa hekari mia moja linamilikiwa na kampuni ya kilimo
ya Tendaji Trade, chini ya Bwana Dunstan Mrutu na Alon Hoven raia wa
Israel.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Rais Kikwete alisifu juhudi za wawekezaji hao kwa
kutumia mbinu za kisasa za kilimo na kuwaasa wanakijiji wa Chikopelo
kujifunza mbinu bora za kilimo hicho cha mboga ili waweze kupata ufanisi
na kuboresha maisha yao. Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaonya
viongozi wa kijiji cha Chikopelo kutoendelea kuuza ardhi yote kwa
wawekezaji na badala yake kutunza na kuilinda kwaajili ya kizazi
kijacho.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)