Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la nyumba mjini Dodma leo - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la nyumba mjini Dodma leo

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mkutano na viongozi wa mifuko ya hifadhi ya Jamii na Shirika la Nyumba la taifa ikulu mjini Dodoma leo.Katika kikao hicho Mheshimiwa Rais aliwapa changamoto viongozi hao  kuunganisha nguvu na kubuni mikakati itakayowezesha kuwapatia watumishi wa umma nyumba za kuishi. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akiongea na mkurugenzi mkuu wa PPF Bwana William Eriyo mjini Dodoma leo baada ya kikao maalumu na viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la Nyumba .
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la Nyumba la Taifa mara baada ya kikao maalumu kilichofanyika ikulu mjini Dodoma leo. viongozi Wengine waandamizi w aliohudhuria kikao hicho Naibu Waziri wa Ardhi Goodluck ole Medeye(watatu kushoto),Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Wanne kushoto),Gavana wa Benki Kuu Professa Beno Ndulu(kulia) na naibu katibu Mkuu Hazina Dr.Servacius Likwelile(kushoto). Katika kikao hicho Mheshimiwa Rais aliwapa changamoto viongozi hao  kuunganisha nguvu na kubuni mikakati itakayowezesha kuwapatia watumishi wa umma nyumba za kuishi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bwana Nehemiah  Mchechu mara baada ya kikao maalumu kilichofanyika ikulu mjini Dodoma leo
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dr.Ramadhani Dau akiteta Jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu mjini Dodoma leo.Picha na Freddy Maro- Ikulu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages