Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Akimkabidhi pesa za Visa mlimbiaji Nelson Brighton kwa niaba ya Mt. Kili Marathon kwenda US
Rais Kikwete na Marie Frances jijini Washington DC
Mwanzilishi wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon Marie Frances mji wa
Bethesda nchini Marekani amemsifu Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama
kiongozi anayependa nchi yake na anayeona mbali. Marie Frances ametoa
sifa hizo hapa mjini Moshi wakati Rais Kikwete akikutana na viongozi wa
Chama Cha Riadha Tanzania (AT) kupanga mikakati ya kufufua riadha nchini
hivi karibuni.
Frances ambaye aliwahi kukutana na Rais Kikwete wakati wa
ufunguzi wa jengo la Tanzania House katika jiji la Washington DC amesema
kuwa ni nadra sana kuona kiongozi wa nchi akikutana na viongozi wa
chama cha mchezo wowote kuzungumzia maendeleo yake. Hii ni miujiza hata
katika nchi kama Marekani.
Marie Frances amemuelezea Rais Kikwete kama mtu wa haiba ya
kipekee mwenye akili na maono ya kuiendeleza Tanzania kufikia malengo ya
Umoja wa Mataifa ya Millenia. “Nilimpenda sana nilipokutana naye jijini
Washington. Ni kiongozi mwenye haiba ya kipekee” alisema Frances ambaye
aliombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja kuanzisha
mbio za marathon nchini Tanzania mwaka 1990.
Marie Frances ambaye alikuwa mkuzaji (producer) wa Miss
Universe pamoja na vipindi vya television huko Hollywwod nchini Marekani
alihamia nchini Misri mwaka 1984 kuafanya kazi ya ABC kama mwandishi wa
bahari. Akiwa nchini Mirsi, Marie Frances alianzisha mbio za Pyramid
Marathon pamoja na Miss Universe ambazo ziitangaza sana nchi ya Misri.
Ni wakati wa matamasha haya balozi wa Tanzania nchini Misri wakati huo
alipomwomba aje Tanzania kuanzisha mbio za marathon ili kuitangaza
Tanzania.
Frances alikuja Tanzania mwaka 1990 na kutaka kuanzisha mbio
za Mt. Meru Marathon lakini alipofika tu mjini Moshi alivutiwa sana na
mlima Kilimanjaro na hivyo kuiamua kuanzisha mbio za “Mt. Kilimanjaro
Marathon” mwaka 1991. Mbio hizi hukimbiwa kila jumapili ya mwisho ya
mwezi wa sita na zitatimiza miaka 22 tarehe 24 Juni mwaka huu.
Mt. Kilimanjaro Marathon zimeshapewa tuzo mbalimbali kama
mbio za kimataifa. Gazeti la Wonders of the World lenye wasomaji zadi ya
million 5 limezipa nafasi ya 2 kama mbio nzuri za kushiriki. Wakati
jarida la kimataifa la Forbes limezipa nafasi ya kwanza kama mbio nzuri
za kukimbia! Marie Frances pia ameanza kuwapeleka wanariadha wa Tanzania
kukimbia nchini Marekani kwa kuwasaidia fedha za Visa za Marekani
pamoja na tiketi za ndege kama inavyoonyesha picha ambapo mkimbiaji
Nelson Brighton anapewa pesa na Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi
Benadetta Kinabo kwenda nchi Marekani mwezi ujao kwa ufadhili wake.Kwa
sasa mbio hizi hufadhiliwa na shirika la ndege la Ethiopia.
Ni katika juhudi zake za kuutangaza mlima Kilimanjatro ndipo
Manispoaa ya Moshi ikaipa jina la Marie Frances Boulevard barabara ya
zamani ya Bustani Ale.
Mt. Kilimajaro Marathon itaanzia
Moshi Klabu tarehe 24 Juni saa kumi na mbili asubuhi ambapo mbio za
kilometa 42, 21, 10 na 5 zitashindaniwa na watalii toka Marekani pamoja
na wakimnbiaji toka Moshi na Arusha.
Wakimbiaji wanajiandikisha kwa wingi Bristol Cottages hotel
iliyopo mkabala na benki ya Standard Chattered karibu na Kilimanjaro
Hospital katika Manispaa ya Moshi.
Imetumwa na:
Grace Soka
Afisa Uhusiano
Mt. Kilimanjaro Marathon 1991
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)