Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda
akizungumza na Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia
ya Serengeti nyumbani kwake Mbezi Beach Teddy Mapunda amefiwa na mdogo
wake marehemu Noela aliyerafiki juzi na kusafirishwa jana kwenda
Shinyanga kwa mazishi, kulia ni Mkurugenzi wa Radio One na ITV B. Joyce
Mhavile.
Rais wa shirikisho la mpira wa muguu
nchini Tanzania TFF Bw. Leodger Tenga akizungunza na mkurugenzi wa
Fullshangweblo Bw. John Bukuku katika msiba wa marehemu Noela jana.
Waombolezaji wakiw akatika msiba huo jana.
Mwili wa Marehemu Noela ukiingizwa nyumbani kwao kwa sala kabla ya kusafirishwa kuelekea mkoani Shinyanga kwa mazishi.
Mama Tunu Pinda akiongoza waombolezaji wakati wa maombo kwa ajili ya marehemu katika msiba huo.
Baadhi ya ndugu wa marehemu wakiwa katika ibada hiyo jana.
Bw. Nestor Mapunda kulia Shemeji wa marehemu Noela akiwa amekaa pamoja na Rais wa TFF Leodger Tenga katikati.
Padri akiongzoa waombolezaji katika swana ya kumuombea marehemu Noela.
Mama Tunu Pinda akimfariji Teddy
Mapunda wakati alipokuwa akimlilia marehemu mdogo wake Noela wakati wa
kutoa heshima za mwisho kwa marehemu nyumbani kwake Mbezi Beach.
Waombolezaji ndugu na jamaa wakilia kwa uchungu wakati wa kuaga mwili wa marehemu.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia
ya Serengeti Ephraim Mafuru katikati akijumuika pamoja na waombolezaji
wengine katika msiba huo.
Mama Pinda akitoa heshima zake za mwisho kwa marehemu Noela .
Teddy Mapunda akifarijiwa na Nandi Mwiyombela huku akilia kwa uchungu wakati akiaga mwili wa marehemu mdogo wake.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia
ya Serengeti Ephraim Mafuru na Rais wa TFF Leodger Tenga wakitoa heshima
zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Noela.
Mkurugenzi wa Fullshangwe John Bukuku akipita kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Noela.
Teddy Mapunda akitoa heshima za mwisho kwa marehemu mdogo wake Noela.
Wazazi wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Noela.Picha Zote Kwa Hisani ya Full Shangwe Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)