Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiof Ali Iddi akimpongeza
Ndugu Said Omar Said { Sugu } kufutai ubunifu wake wa Gari iliyopewa
jina la Sugu 11 .Balozi Seif aliikagua gari hiyo baada ya kukagua
maonyesho ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na Ile ya Nguvu za
Atomiki Tanzania hapo Tunguu.
Afisa wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia { actech } Bwana Saleh
Mikidadi akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
balozi Seif Ali Iddi aliyefungua rasmi Ofisi ya Tume hiyo pamoja na ile
ya Nguvu za Atomiki iliyopo katika Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jmauhuri ya Muungano liliopo Tunguu.
Nyuma ya Afisa Mikidadi ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Muungano Mh. Makame Mnyaa Mbarawa.
Nyuma ya Afisa Mikidadi ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Muungano Mh. Makame Mnyaa Mbarawa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia
bidhaa zilizotengenezwa na moja ya Kikundi cha wajasiri amali cha Kijiji
cha Paje kwenye maonyesho ya uzinduzi wa Ofisi za Tume ya Sayansi na
Teknolojia na Ile ya Nguvu za Atomiki hapo Tunguu
Bidhaa hizo zimetengenezwa kwa mali Ghafi ya Mwani chini ya usimamizi wa
wataalamu wa Taasisi ya Uchunguzi wa Sayansi ya Baharini ya Chuo Kikuu
cha Dar es salaam.
---
Uongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania {costech}
umeombwa kushajiisha Wasomi hasa Vijana wa Vyuo Vikuu Nchini kupenda
kufanya tafiti mbali mbali zitakazojenga Mazingira ya kumuondoa
Mtanzania kwenye matatizo yanayomkabili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa ombi hilo
katika Hafla fupi ya uzinduzi wa Ofisi ya Tume hiyo ilyofanyika hapo
Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Balozi Seif alisema Tafiti kama hizo ambazo zitakuwa na uhusiano wa moja
kwa moja na Mwananchi zinaweza kusaidia kupata Maendeleo kwa kasi zaidi
katika Kipindi kifupi kijacho.
Alisisitiza kwamba Serikali kwa upande wake iko tayari kwa namna yoyote
ile kutumia vyema matokeo ya Tafiti zinazofanywa na Wazomi wazalendo.
Hata hivyo Balozi Seif alieleza kuwa yapo baadhi ya matokeo ya Tafiti
hubakia kuwa siri kwa Taifa lakini mengine yanastahiki kutolewa kwa
Wananchi ili waelewe kinachoendelea kwenye maisha yao.
Balozi Seif alieleza kwamba wakati umefika kwa Makampuni pamoja na
Viwanda vya hapa Nchini kujenga Utamaduni wa kutoa kazi zao za Utafiti
kwa Tume hiyo ili ijipatie fedha za kuendesha shughuli zake za utafiti
kama Nchi nyengine zilizoendelea.
Alieleza kwamba Tanzania imepania kuleta maendeleo kwa Wananchi wake
kutokana na uamuzi wake wa kutenga Jumla ya shilingi za Kitanzania
Bilioni Thalathini { 30,000,000,000/-} kwa ajili ya Utafiti na Maendeleo
kwenye Bajeti yake ya Mwaka 2010/2012.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Maendeleo bila ya Sayansi na Teknolojia
hayapatikani kwani masuala hayo mawili yanakaribiana katika utekelezaji
wake.
Akizungumzia Tume ya Taifa ya nguvu za Atomu Balozi Seif alielezea
kufarajika kwake kutokana na mipango m,izuri ya Taasisi hiyo kuhudumia
Zanzibar katika masuala ya usimamizi wa matumizi salama ya Mionzi.
Balozi Seif alisema ushirikiano wa pamoja wa Taasisi hiyo,Wizara ya Afya
Zanzibar na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani katika kuanzisha mradi
wa Matibabu ya Saratani katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja unafaa
kuungwa mkono.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameishukuru
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa wa
kusogeza karibu na Wananchi shughuli za Ofisi ya Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Tume ya Taifa ya Nguvu za Atomu.
Katika Taarifa yake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania
Profesa Iddi Suleiman Nyangarika Mkilaha alisema Taasisi yake
itaendelea kutoa Elimu sahihi ya matumizi ya Mionzi.
Profesa Nyangarika alisema Taaluma hizo kwa sasa itazingatia zaidi
katika sekta ya Viwanda pamoja na Vituo vya Afya ambavyo vinatumia Vifaa
vyenye mazingira ya Nguvu za Atomiki.
Mkurugenzi huyo wa Tume ya Nguvu za Atomiki alifahamisha kwamba katika
kupanua zaidi huduma zake Taasisi hiyo itaendelea kupima Mionzi katika
Mimea ili kujua kiwango sahihi cha kulinda Vyakula kwa ajili yamatumizi
bora kwa Wanaadamu.
Mapema Waziri wa Mawasiliano,Sayansina Teknolojia wa Serikali ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Makame Mnyaa Mbarawa alisema Wizara
hiyo itaendelea kushirikiana na Wataalamu wa ndani na nje ili kuona
Tafiti zinazofanywa zinatmika kwa walengwa ambao ni Wananchi.
Alisema Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na ile ya Nguvu za
Atomiki zimeanzishwa zikiwa na wajibu wa kusimamia tafiti na nguvu za
Atomiki Nchini kwa kushirikiana na Taasisi za Kanda na zile za
Kimataifa.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi Ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)