Mafunzo ya uokoaji kwenye maji kufanyika Juni 27-29 jijini Dar es salaam - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mafunzo ya uokoaji kwenye maji kufanyika Juni 27-29 jijini Dar es salaam

Bwana Alex Mwaipasi katibu Mkuu wa chama cha kuogelea akizungumzia maonyesho yatakayokuwa maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya jinsi ya kutumia maji wakiwa salama ikiwa ni pamoja na kujua jinsi ya kujiokoa unapopata dharura ya kuzama kwenye maji kushoto ni John Belele Mwenyekiti wa chama cha kuogelea, Maonyesho hayo yatafanyika kwenye viwanja vya Tanganyika International School Upanga jijini Dar es salaam  kuanzia Juni 27-29 

TAARIFA YA CHAMA CHA UOKOAJI

Tanzania Life Saving Society (TALISS) ni taasisi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ambayo jukumu lake kubwa ni kuzuia/kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na maji, kwa njia ya kutoa elimu kwa jamii jinsi ya kuishi salama karibu/ndani ya maji, pamoja na kusimamia maswala ya usalama kwa watumiaji wa maji ya wazi (Open water) na mabwawa (Swimming pools).

Katika kuendelea kutimiza wajibu wa kuelimisha jamii, Tanzania Life Saving Society (TALISS), kwa mara ya kwanza inazindua Wiki ya Kuzuia Vifo Katika  Maji Kitaifa (NATIONAL DROWNING PREVENTION WEEK) utakaofanyika katika shule ya kimataifa ya Tanganyika (IST) iliyopo upanga Dar es salaam, kuanzia tarehe 26 mpaka tarehe 30 Juni, 2012 kila siku saa 8:00 mchana mpaka saa 11:00 jioni, sambamba na hilo TALISS pia itakuwa inaadhimisha miaka 20 ya kuzaliwa kwake.

Katika uzinduzi huo tutatoa semina na kufanya maonesho mbalimbali, ambapo kusudi kuu la tukio hilo ni kukuza na kueneza elimu ya uokoaji na usalama katika maji hapa nchini.
 
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa ushirikiano wenu.

 Wako katika uokoaji wa maisha,

ALEXANDER H. MWAIPASI
KATIBU MKUU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages