HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA ELIMU ALIPOFUNGA CLINIC YA SPRITE HASHEEM THABEET 2012 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA ELIMU ALIPOFUNGA CLINIC YA SPRITE HASHEEM THABEET 2012

 Mhe. Phillipo Mulugo (MB)Naibu Waziri wa Elimu akisoma hotuba yake
 Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania Phares Magesa
(Wa Pili Kulia,Brand Manager msaidizi wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro(Wa Kwanza Kushoto)Afisa Utamaduni, Ubalozi wa Marekani,  Danna Banks(wa kwanza Kulia),Brand Manager msaidizi
 wa Coca Cola  Bibi Warda Kimaro(Wa Kwanza Kushoto),Hashim Thabeet(Wa Pili Kushoto)
 Baadhi ya Vijana Walioshiriki Clinic Ya Sprite Hasheem Thabeet 2012
---

Mkurugenzi wa Michezo
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania Ndugu 
Phares Magesa
Afisa Utamaduni, Ubalozi wa Marekani, Danna Banks
Brand Manager msaidizi wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro
Hasheem Thabeet ,
Viongozi wa TBF,
Makocha, 
Wachezaji
wadau wote wa michezo.

Kwa niaba ya Serikali na kwa niaba yangu binafsi napenda kuchukua nafasi hii  kuwashukuru TBF kwa kazi kubwa walioifanya ya kuakikisha mafunzo haya  yanafanyika   katika kiwango kizuri , zaidi napenda kuwashukuru Coca cola kupitia  kinywaji cha Sprite kwa kuendelea kufadhili mchezo wa Mpira wa kikapu hasa katika  ngazi ya Vijana wadogo, pia nawashukru sana watu wa Marekani kupitia Ubalozi wao  hapa Dar Es Salaam kwa kusaidia kuendeleza vijana wetu kupitia mchezo wa kikapu.

Kipekee na penda kumpongeza Hasheem Thabeet kwa kuonyesha thamani yake katika  mchezo wa Mpira wa Kikapu na kukubali kutumia muda wake kwa ajili ya Vijana  wadogo  kuwapa mafunzo na kuinua ari kwa vijana wetu  ili nao wapate kuwa na ndoto  na  kufika pale alipo yeye

Nimatumaini yangu mafunzo haya mmeyapokea vizuri mtayazingatia na mtakapo rudi  kwenye shule zenu nanyi mkawe mabalozi wazuri na walimu kwa wenzenu ambao  hawakupata nafasi kama hii mliyoipataMikoa iliyoshiriki kliniki hii ya mwaka huu ni  Mwanza, Tanga, Dodoma,Kilimanjaro, Arusha, Unguja, Pemba na mkoa mwenyeji wa  Dar es Saalaam hivyo basi ni matumaini yangu mwakani mikoa yote ya Tanzania bara  na visiwani itashiriki, naomba wafadhili wajitokeze zaidi kuunga mkono jitihada za Cocacola na Hasheem Thabeet ili tuibue vipaji vingi zaidi katika kikapu.

Ndugu zangu serikali ipo pamoja nanyi katika michezo  kama mnavyofahamu wote  kuwa mashindano ya Umiseta na umitashumta yamerudishwa rasmi mashuleni,    hivyo mafunzo haya waliyopata vijana hawa basi yatasaidia kuwaimarisha kimbinu za  kimchezo na ni matumaini yangu mikoa iliyoshiriki hapa itafanya vizuri kwenye 
mashindano yajayo ya shule za sekondari na msingi.

Serikali itaendelea kushirikiana na vyma vya michezo vyote nchini katika kuhakiksha  michezo inaimarika mashuleni ikiwa ni pamoja kupeleka walimu wengi zaidi  wakasomee  taaluma hii katika vyuo vyetu mbali mbali, ikiwa ni sambamba na kuongeza  uwezo wa vyuo vyetu vya ualimu  kufundisha michezo.

Narudia tena wito wangu kuwa michezo ni sehemu muhimu ya kujenga vijana wetu  kiafya, kielimu na kimaadili na hata kiuchumi hivyo basi ni jukumu la kila mmoja wetu,  wanamichezo, wazazi, walezi na wakuu wa shule zote nchini kuhakisha vijana  wanapatiwa fursa ya kushiriki katika michezo.

Nafahamu kuwa changamoto ya miundombinu ya michezo bado ni tatizo kubwa katika  nchi yetu, hivyo basi Serikali itafanya kila jitihada kushirikiana na wadau wengine  kuhakikisha tatizo hili linashugulikiwa ipasavyo katika ngazi zote.

Maombi yenu kwa serikali ya kuomba mpewe kipaumbele katika ujenzi wa uwanja  mkubwa wa ndani wenye hadhi ya kimataifa kama wezenu wa soka na riadha  wanavyofaidika na uwanja mkuu wa Taifa, nimeyachukua na nitayafikisha katika ngazi  husika ili yaweze kushugulikiwa.

Nawashukuru sana wadhamini wa mafunzo haya kampuni ya Cocacola kupita SPRITE  naHasheem Thabeet na nitoe wito kwa wanamichezo wengine Tanzania kuiga mfano  wa Hasheem Thabeet wa kurudisha fadhila kwa jamii nzima ya watanzania na nia yake  njema ya kuona vipaji vingine vinaibuka Tanzania. Niwatakie heri katika mafunzo mengine kama haya yatakyofanyika Arusha juma lijalo. Natoa wito tena kwa makampuni mengine yajitokeze kudhamini michezo na hususani  mchezo wa kikapu. Niwatakie Safari njema wale wote watakaosafiri kurudi mikoani na niwashukuru wote  kuanzia Walimu wenu,Wazazi kwa kuwapa ushirikiano mzuri katika kuchangia kufanikisha  malengo yenu.

Asanteni kwa kunisikiliza na sasa nimeyafunga rasmi mafunzo haya ya  
SPRITE HASHEEM THABEET CLINIC 2012.

Mhe. Phillipo Mulugo (MB)
Naibu Waziri wa Elimu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages