Hatimaye Dr. Ulimboka apelekwa Afrika ya Kusini kutibiwa mapema leo. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Hatimaye Dr. Ulimboka apelekwa Afrika ya Kusini kutibiwa mapema leo.

 Gari la wangonjwa la AAR ambalo lilimbeba Dk. Ulimboka likiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Baadhi ya wanaharakati na wauguzi wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kulaani kitendo cha kikatili alichofanyiwa daktari huyo.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka leo mchana alifikishwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya madaktari kubaini kuwa ana mtatizo ya kitabibu yanayomkabili likiwemo la mtikisiko wa ubongo.

Mwenyekiti huyo alifikishwa uwanjani hapo majira ya saa 8.30 na ndege aliyosafiri nayo iliondoka saa 10.15. Uwanjani hapo kulikuwa na wanaharakati ambao walikuwa na mabango, kinyume cha matarajio ya wengi walizani kuwa angeteremshwa na kuingizwa na machela Uwanjani hapo lakini gari lililombeba lilipita moja kwa moja hadi ndani ya uwanja huo. Chanzo: Global Publishers Info

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages