Mcheza
sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ameahidi kuleta wacheza sinema wenzake
na kushiriki kwenye mbio za mwaka kesho za mt. Kilimanjaro Marathon zitakazokuwa
zinatimiza miaka 23 tangu zianzishwe mwaka 1991.
Lorenz
aliyekimbia mbio za mwaka huu ambazo zilipewa jina la “mbio za kutimiza miaka
50 ya uhuru wa Tanganyika” na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) amesema kuwa
atakuja na timu yake ya wapiga picha ili kupiga picha vivutio kadhaa vya Tanzania
ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro. Qwiji hili la sinema za Santorini Blue,
The Great Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi ameelezea kuipenda sana
Tanzania.
“Sikutegemea
kuikuta nchi nzuri kama hii” alisema mcheza sinema huyo ambaye ameshawahi
kuchaguliwa zaidi ya mara 4 kugombea tuzo maarufu za Oscar. “Sasa nimeamini kuwa
mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania na nitautangaza katika sinema zangu zote”
aliendelea kusema Deidre Lorenz.
Mcheza
sinema huyu ambaye ameingia kwenye mkataba na kampuni kubwa ya Google hivi karibuni
ili kuuza sinema zake katika mtandao aliielezea Tanzania kama nchi nzuri na yenye
watu wakarimu sana.
Mbio
za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances anayetoka
katika jiji la matajiri la Bethesda nchini Marekani baada ya kuombwa na balozi
wa zamani wa Tanzania nchini Misri. Tangu kuanzishwa kwake mbio hizi zimekuwa
zinaleta watalii matajiri katika mji wa Moshi kupanda mlima Kilimanjaro na kukimbia
mbio hizi zinazojulikana kama Seven Continental Races.
Hakuna
masharti yote ya kukimbia mbio hizi na watanzania wanaoshiriki katika mbio hizi
huwa hawatozwi pesa za kiingilio.
Kwa
kutambua mchango wake katika uchumi wake Manispaa ya Moshi iliibadilisha
jina barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie Frances Boulevard ili
kumuenzi mama huyu aliyejitolea maisha yake kuutangaza mlima Kilimanjaro.
“Kila
siku napokea ujumbe kutoka nchi mbalimbali niende huko kuanzisha mbio za
marathon lakini kwa sasa basi” alisema mama huyo aliyekuwa mtayarishaji wa
vipindi vya televisheni ya ABC kabla ya kunzisha Mt. Kilimanjaro Marathon.
Alisema
kuwa mwaka jana yeye na Rais wa klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon mtanzania
Onesmo Ngowi walifanya makubaliano ya Ethiopia Airlines (ET) jijini Addis Ababa
kuzifanya mbio hizo kuwa za kimataifa zaidi. “ET walikubali kutoa ufadhili kwetu
na pia kugharamia kushiriki kwetu katika mbio za New York Marathon, Boston
Marathon na Los Angelos Maratthon ili kuitangaza vyema Tanznaia” alibainisha
Frances.
Katika
makubaliano hayo, Ngowi na Frances pia wataanzisha mbio za “King Solomon
Marathon” zitakazofanyika katika jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.
Deidee
Lorenz amefungua pazia kwa watu mashuhuri kushiriki katika mbio za marathon nchini
Tanzania na ni jukumu la Watanzania kuchangamkia fursa zinazoletwa na ujio wao.
Imetumwa
na:
Grace Soka
Afisa Uhusiano
MT. KILIMANJARO MARATHON 1991
|
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)