Waziri
wa Usalama wa ndani wa Kenya, Profesa. George Saitoti, (pichani)
amefariki dunia kwa ajali ya Helikopta, aliyokuwa akisafiria akiwa
katika safari ya kikazi akielekea Kisumu, akiwa na Naibu Waziri wake
Orwa Ojode na kupata ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi katika eneo la
Ngong, nchini humo na kufariki dunia.
Habari
zilizoufikia mtandao huu wa Lukaza Blog, zinasema
kuwa ajali hiyo, imetokea katika maeneo hayo ya Ngong, katika milima ya
Magharibi mwa Jiji la Nairobi nchini nchini Kenya.
Mpaka
sasa bado Serikali ya Kenya haizungumzia ajali hiyo iliyowapoteza
Waziri na Naibu wake pamoja na watu wanne na kufanya jumla waliofariki
katika ajali hiyo kufikia watu Sita.
Profesa
Saitoti, alikuwa ni mmoja kati ya watu waliojitokeza kutangza kugombea
urais katika uchaguzi wa Rais utakaofanyika hivi karibuni nchini humo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)