Afisa
mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin akikabithi
radio ya solar kwa mkazi wa kijiji cha Ololosokwan wakati wa ziara ya
kutembelea mradi wa Radio jamii ulioanzishwa chini ya udhamini wa
Airtel kwa kushirikia na UNESCO, Radio zaid ya 200 zilikabithiwa kwa
wakazi wa kijiji hapo, uzinduzi wa Radio hii utafanyika mwishoni mwa
mwenzi juni,
Afisa
mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin akionyesha
jinsi gani radio ya solar inavyofanya kazi mara baada ya kukabithi
Radio 200 kwa wakazi wa kijiji cha Ololoskwan wakati wa ziara ya
kutembelea mradi wa Radio jamii ulioanzishwa chini ya udhamini wa
Airtel kwa kushirikia na UNESCO, Ololosokwani Radio inategemea
kuzinduliwa mwishoni mwa mwenzi juni, wakishuhudia kushoto ni
mwakilishi wa Airtel Ahmed Juma katika ni Yannick Ndoinyo Mkurugenzi
mtendaji IrkiRamat Foundation (RAMAT
wafanyakazi
wa Airtel Dua Kazimoto na Mercy Nyange wakiwa katika picha na wanawake
wafanyabiashara wa vikundi vidogovidongo wa kijiji cha Ololosokwani
wakati wakati walipotembela mradi wa radio unotegemea kuzinduliwa
mwishoni mwa mwenzi Juni
wanakijiji
cha Ololoskwan na wawakilishi wa UNESCO na Airtel wakiwa katika picha
ya pamoja wakati walipotembela mradi wa radio unotegemea kuzinduliwa
mwishoni mwa mwenzi Juni
XXXXXXXXX
Airtel yashirikiana na UNESCO kuanzisha Radio za jamii Nchini
* Mikoa zaidi ya 10 nchini kufikishiwa Radio za jamii
* Lengo ni kukuza sekta ya mawasiliano hususani maeneo
yaliyo na chagamoto za kijamii.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na UNESCOwamejiunga
kuendeleza sekta ya mawasiliano nchini na kuhakikishahuduma za
mawasiliano ya radio zinawafikia wananchi wengi hasa walewanaoishi
kwenye maeneo ya vijiji zinavyokumbwa na changamotonyingi za kijamii
pamoja na kukosekana kwa huduma za radio.
Airtel
na UNESCO kwa kutambua umuhimu wa mawasiliano katika karne hiiya 21 na
katika kuhakikisha jamii inapata habari za uchumi, siasa naza kijamii
ambazo ndizo nyenzo muhimu kwa maendeleo ya jamii yeyoteduniani
wameonelea ni vyema kwa kushirikiana na jamii husika kuanzisharadio za
jamii (community Radios) ili kutoa nafasi kwa wananchi kupataelimu
mbalimbali kwa kupitia Radio hizi zitakazoenea nchini kote.
Lengo
kubwa la kuanzisha radio hizo ni kwasababu maeneo mengi yamekosahuduma
hizi muhimu za mawasilino na hivyo kujikuta kuwa kwenye mifumoduni ya
kijamii kama vile ukiketwaji wa wanawake, elimu duni, imani
za kishirikina, Umaskini , unyanyasaji wa kijinsia, kuenea kwa kasikwa ugonjwa wa ukimwi na matatizo mengine mengi.
Akiongea
wakati walipotembelea Radio iliyopo Ololosokwani msimamizi wamradi na
Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema, "Airteltunajisikia
furaha kuwafikia wananchi na wateja wetu kwa kupitiamtandao wetu
uliompana zaidi, tunaamini kwa kupitia radio hizi elimu itatolewa kwa
jamii, upatikanaji wa habari za kiuchumi na biashara kutawezesha
kuboresha shughulili za kiuchumi katika maeneo husika na nchi kwa
ujumla, pia radio hizi zitawapa wakazi kufahamu hali ya kisiasa nchini
na kupata habari mbalimbali za ndani na nje ya nchi tofauti na ilivyo
sasa.
Airtel
tunawajali sana na ndio maana ndio mtandao pekee unaopatikanahapa
kijijini Ololosokwani , na leo hii pia bado tumepiga hatuanyingine kwa
kushirikiana na wenzetu wa UNESCO kufikisha huduma yaradio pekee ya
Tanzania kijinini hapa ambayo masafa yake yatasikikahadi vijiji vya
jirani"
Airtel
tunaendelea kutimiza dhamira yetu kwa kushirikiana na serikaliya
jamuhuri ya muungano chini ya wizara husika kuhakikisha
tunachangiakatika kufikisha huduma hii muhimu kwa watanzania na kuleta
mabadilikoya kiuchumi na kijamiii katika maeneo yanayoonekana ni duni na
ambayohayajafikiwa.
Naye
Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Aminalisema"
mradi wa radio hapa kijiji cha Ololosokwani utawawezeshawakazi wa hapa
kupata mawasiliano ya karibu na sehemu mbalimbali zaTanzania,
kutawawezesha kujifunza mambo mapya, kutangaza mila nadesturi za
kimasai, kuweza kufahama mambo ya utawala bora na kuwezakuhoji viongozi
wao, kupata habari mbalimbali, na pia kuelimishawamasai kuendeleza
tamaduni zao na maendeleo kwa ujumla.
"Tunawashukuru
wenzetu wa Airtel kwa kushirikiana nasi katikakuuanzisha mradi huu kwa
kupitia radio hii tutaweza kufikia vijiji 14pindi tutakapoanza kurusha
matangazo"alisema Bw, Al AminBw Al-Amin pia aliongeza kwa kusema "Pamoja
na mradi wa radio piatumeweza kuanzisha multimedia center
itakayowasaidi wakazi wa kijijinihapa na shule ya sekondari
iliyopokaribu kuweza kutembelea tovutimbalimbali na kuweza kupata huduma
za internet"
Vile
vile tumeanzisha mradi wa kuboresha nyumba zakimasai kuondoa moshi na
kuongeza mwanga na tutajenga nyumba mbili za mfano hivyo tunategemea
wakazi wa hapa watajenga nyumba za makazi zilizo na kiwango kulinganisha
na sasa na mradi mwengine ni wa kuboresha maziwa ya ngome na nyama na
kuweza kutengeneza viwanda vidogo na kutengeneza jibini na mwisho
tunaanzisha mradi wa solar utakao wawezesha wakazi wahapa kupata um eme"
aliongeza Al Amin.
Miradi
yote hii imeanzishwa baada ya kuanza mradi wa radio na kuona maeneo
mengine ambayo tunaweza kuyaboresha na kuleta mabadiliko kwa wakazi wa
hapa alimalizia kwa kusema Bw, Al Amin
Akiongea
na waandishi wa habari mkazi wa kijiji cha
ololoskwanialiyejitambulisha kwa jina la bi Nekisho Ndoinyo alisema hapa
kijijini kwetu hatuna radio ya Tanzania tuaamini kabisa kwa kuanzishwa
radio hii
kutaleta mafanikio makubwa kwa vikundi vya kina mama na wakazi wa hapa
kutangaza biashara zao, tutaweza kupata taarifa mbalimbali , tutaweza
kutangaza mila yetu ya kimasai, watoto wetu watapata elimu na kuweza
kujua nafasi mbalimbali za shule na kazi, hivyo basi nachukua fulsa hii
kuwahamasisha wanakijiji kushiriki katika vipindi vya radio pale
itakapoanza kurusha matangazo yake, tumefurahi sana kuweza kupata
mawasiliano haya ya radio na tunashukuru sana Airtel na UNESCO kwa
jitihada hizi.
Kwa
upande wake mkazi wa kijiji cha ololosokwani bi Kootu Tome aliongeza
kwa kusema tatizo kubwa la kijiji hicho ni mgogoro wa Ardhi na
wawekezaji kuvamia maeneo yao hivyo naamini radio itatoa mwanga kwa
jamii na kuweza kutambua haki yao ya kimsingi.
Mradi
huu wa Radio za jamiii unaosimamiwa na UNESCO kwa kushirikiana na
Airtel unategemea kufunguliwa rasmi mwishoni mwa mwenzi Juni kwa
kuzindua kituo cha Radio kilichopo Ololosokwani Arusha. Mikoa mingine
itakayofikishiwa radio za kujamii ni pamoja na Kyela Mbeya, Uvinza
Kigoma, Pemba na maeneo mengi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)