WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na wafanyakazi wa Tazara, kulia ni naibu wake Dk. Charles Tizeba, na kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Tazara Damas Ndumbalo.
Naibu Mkurugenzi wa Tazara Damas Ndumbalo akifafanua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi.
Mmoja ya washiriki katika mkutano akichangia hoja.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tazara wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe.
Wafanyakazi wa Tazara wakishangilia ahadi za Waziri wa Uchukuzi.
--
WAZIRI
wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ameapa kulinusuru Shirika la Reli ya
Tanzania na Zambia (Tazara) kwa kufumua uongozi uliopo na kuweka
uongozi mpya sanjari na kubadiliha mfumo wa uendeshaji shirika hilo.
“Matatizo
yanayoikabili Tazara ni uongozi mbovu hakuna cha Zambia wala
Tanzania,hili tutalitafutia mwarubaini kwa hapa nchini lipo chini yangu
na kwa Zambia ni la mamlaka nyingine,”alisema Mwakyembe.
Awali
Katibu Mkuu wa (Trawu) Erasto Kiwele alitoa madai ya wafanya kazi
ambapo alisema wanadai mishara ya miezi miwili na kumtaka Waziri Dk
Mwakyembe kutumia uwezo wake kuwaondoa kwenye nyadhifa zao Mkurugenzi
Mtendaji wa Tazara na Naibu wake.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)