Wanafunzi chuo cha Mkwawa Iringa wakiwa wamepiga kambi nje ya benki ya NMB Iringa kushinikiza kuingiziwa fedha zao .
NA PAULINE KUYE IRINGA
Wanafunzi wa chuo kikuu cha mkwawa mkoani iringa leo mchana wamefanya maandano na kuzuia barabara ya kuu iendayo IRINGA -Dodoma KATIKA maeneo ya posta.
Wanafunzi hao wamefunga barabara hiyo wakati wakifanya maandamano kutokanana na kucheleweshwa kwa fedha za kujikimu ambazo hutolewa na bodi ya mkopo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi
hao wamesema kuwa wameshapeleka malalamiko yao kuanzia ngazi ya chuo
hadi kwa mkuu wa mkoa lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Maaandamano
hayo yalisambaratika ilipotokea gari ya askari wa kuzuia ghasia na
kuwataka wanachuo hao waache kuzuia barabara hiyo kwani barabara hiyo ni
huduma ya jamii.
Kutokana
na amri hiyo ilibidi waanze kuelekea ofisini kwa mbunge wa Iringa mjini
MCH.PETER MSINGWA ambapo mbuge huyo aliwatuliza na kuwaambia wanafunzi hao kuwa na subira kwani kuanzia kesho malipo hayo yatakuwa tayari.
Baaada ya maelezo ya mbunge kuwalizisha wanachuo
hao waliamua kurudi chuoni huku wengine wakisema kama mkuu wa chuo
hicho hata waambia hatma ya pesa hizo basi leo watakesha ofisini kwake.Habari Kwa Hisani ya Full Shangwe Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)