Kampuni ya mawasiliano inayoongoza Tanzania, Vodacom leo imezindua
promosheni kwa ajili ya wateja wake ambapo kuanzia leo hadi mwisho wa
wikiendi watapata nyongeza ya asilimia hamsini kila mara wanapoongeza
muda wa maongezi wa kuanzia Tsh1000.
Katika taarifa kwenye vyombo vya habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza alisema promosheni hii imetokana na kuguswa kwa wateja na kampeni iliyozinduliwa hivi karibuni ya WAJANJA ambayo imeonyesha kupendwa na kutumiwa sana na wateja wao kwenye matumizi ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi SMS na kuperuzi kwenye internet.
“Tunajivunia tunapowaona wateja wetu wakifurahi na kuendelea kutumia huduma zetu na hii promosheni inanuia kuwapa thamani zaidi yapesa zao wakati huu wa wikiendi ikiwa ni fursa kubwa kwa familia kufanya shughuli kadha wa kadha,” alisema Bwana Meza.
Nyongeza hii ya salio ya asilimia 50 inaweza kutumika kwa kutuma ujumbe mfupi, kupiga simu na kuperuzi internet kupitia simu za mkononi na pia promosheni hii ni kwa ajili ya wateja wanaotumia Mpesa kununua muda wa maongezi.
Wateja pia wanaweza kuangalia salio la nyongeza hii kwa kubonyeza *102*02#
· Vodacom TZ ndio mtandao unaoongoza katika kutoa huduma za mawasiliano nchini, ikiwapa wateja wake huduma mbali mbali za kibunifu zinazolenga matumizi ya simu na deta.· Kampuni hii imeimarisha huduma zake kwa wateja kupitia njia mbali mbali kama vile kutoa usaidizi wa kitechnolojia kuwapa uzoefu wateja wanaotumia simu za kisasa mara moja

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)