Afisa wa Masuala ya Umma Ubalozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dana L. Banks
--
Habari
au taarifa ni nguvu. Ni watu wachache sana wanaoweza kuishi,
kuiwajibisha serikali yao na kuwaelimisha watoto wao bila kuwepo kwa
mtiririko huru na thabiti wa habari.
Raia
wanahitaji taarifa sahihi na zenye kuaminika, katika wakati sahihi.
Vivyo hivyo kwa wafanyabiashara, masoko na hata serikali.
Watumiaji wa leo wa taarifa duniani kote wanataka kupata tarifa wanazozihitaji katika sekunde kadhaa na wala si saa au siku kadhaa.
Watumiaji wa leo wa taarifa duniani kote wanataka kupata tarifa wanazozihitaji katika sekunde kadhaa na wala si saa au siku kadhaa.
Kupanuka kwa njia mbalimbali za
kijamii za kusambaza habari hasa kwa kupitia teknolojia ya kisasa
miongoni mwa watu na hata vyombo vya habari vyenyewe, kunaashiria hamu
kubwa ya umma kupata taarifa wakati wote.
Jambo hili limekuwa kama sehemu
muhimu ya maisha ya kila siku. Watu wengi hawawezi kuendesha shughuli
zao za kila siku za kujikimu, kuwajibisha serikali zao au kuelimisha
watoto wao bila kuwa mtiririko huru na thabiti wa habari. Raia
wanahitaji taarifa sahihi na zenye kuaminika kwa wakati sahihi.
Uhuru wa vyombo vya habari huzifanya
jamii pamoja na uchumi wake kuchangamka, kuimarika na kustawi. Pale
ambapo mtiririko huru wa habari umekatwa basi watu mmoja mmoja, jamii na
hata uchumi huathirika vibaya.
Karne ya 21 imeleta mapinduzi makubwa ya mawasiliano na upashanaji habari. Mataifa na watu ambao hapo awali walikuwa wametenganishwa na mipaka ya nchi zao, wanaunganishwa moja kwa moja kwa kupitia mtandao wa mawasiliano wa Internet.

Aidha, ni wao ndio wanaoandika na
kuueleza ulimwengu mzima kuhusu hali zao. Kama tulivyoona katika kipindi
cha mwaka mmoja uliopita, jamii ambazo zinakandamiza waandishi na
vyombo vya habari, haziwezi tena kufanya hivyo kwa muda mrefu kabla ya
raia hawajaweza kusambaza taarifa zao na kujenga mitandao mikubwa ya
upashanaji habari kwa kutumia njia za kisasa na thabiti za upashanaji
habari kwa kupitia mtandao (social media tools).
Mtandao wa Internet umepanua
majadiliano na ubadilishanaji mawazo baina ya watu wa mataifa yote
duniani. Kwa kiwango kikubwa mtandao huu wa mawasiliano ulichangia
kuangushwa kwa tawala kandamizi Kaskazini mwa Afrika mwaka jana na ndio
unawezesha raia katika nchi za Magharibi- ikiwemo Marekani - kufuatilia
utendaji wa serikali zao.
Uhuru wa vyombo vya habari umejumuishwa katika Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu la Mwaka 1948 linaloeleza kuwa "Kila mtu ana haki ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yake; haki hii inajumuisha uhuru wa kuwa na maoni bila kuingiliwa na kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa na maoni kwa kupitia njia yoyote ya upashaji habari bila kujali mipaka ya nchi."
Uongozi katika vyombo vya habari, iwe ni vile vya uchapishaji, utangazaji, mtandao wa internet na mitandao ya kijamii ni muhimu katika maendeleo ya uhuru wa habari. Hasa katika kuvifanya vyombo hivi kutokuwa vyombo vya kuisemea serikali bali vyombo huru vya ufuatiliaji.

Uongozi ndiyo unaotoa dira na misingi
ya kimaadili kwa uandishi wa habari na hivyo kujenga imani ya umma kwa
vyombo hivyo. Viongozi katika tasnia ya habari Tanzania ni wale wote
wanaowafundisha, kuwaongoza na kuwatia moyo waandishi wa habari wa
kizazi kijacho kwa kupitia njia mbalimbali za kuwaendeleza (professional
development). Viongozi hawa wanaongoza kwa mifano wakiwezesha vyombo
vya habari kutekeleza wajibu wake wa kuimarisha utawala wa kidemokrasia.
Kwa upande mwingine, watu katika taifa lolote wanaponyimwa haki na uhuru wao wa kupata habari husababisha kuenea kwa taarifa za upotoshaji, uvumi na dhana potovu.
Marekani ina fahari kubwa kushirikiana na vyombo vya habari vya Tanzania katika jitihada za kuwapatia Watanzania taarifa sahihi na zinazotolewa kwa wakati na kuhimiza na kuimarisha demokrasia.

Vyombo vya habari vinashiriki
kikamilifu na kuchangia katika kuweka kumbukumbu ya jitihada za kujenga
demokrasia kwa kupitia chaguzi za kidemokrasia, mjadala wa katiba mpya
na hata harakati za kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika
kufanya maamuzi. Kuendelea kuimarika kwa uongozi na viwango vya utendaji
katika vyombo vya habari kutawezesha kulinda mafanikio yaliyofikiwa na
kupatikana kwa mafanikio zaidi katika nyanja hizi na nyinginezo.
Wakati siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikikaribia, Marekani inapenda kusisitizia dhamira yake ya dhati ya kuona kuwa waandishi huru wa habari wanafanya kazi yao bila hofu yoyote.
Wakati siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikikaribia, Marekani inapenda kusisitizia dhamira yake ya dhati ya kuona kuwa waandishi huru wa habari wanafanya kazi yao bila hofu yoyote.
Aidha, tunawakumbuka na kuwaenzi
waandishi wa habari, waandishi katika mitandao (bloggers) na raia jasiri
ambao wamejitolea maisha, afya na uhuru wao ili watu wengine waweze
kufahamu ukweli. Hali kadhalika, tunathamini na kuenzi mchango wa vyombo
huru vya habari katika kujenga demokrasia, uwazi na uthabiti wa jamii.
Tunatambua kuwa, kama wakala wa mabadiliko, viongozi wa vyombo vya habari wanachangia pia katika kuimarisha utawala bora na maendeleo ya kiuchumi kwa kujenga jukwaa litakalowawezesha wanajamii kutoa sauti yao na hivyo kuwezesha kujengwa na kukua kwa jamii iliyo wazi zaidi.
Mjadala wa kitaifa nchini kote
Tanzania utaimarishwa pale ambapo kila raia atasaidia kuiimarisha kada
ya uandishi wa habari katika misingi ya maadili na uhuru na hivyo
kuiwezesha kuchangia zaidi katika maendeleo ya taifa.
Tunawapongeza waandishi wa habari wa
Tanzania kwa kujitoa kwa dhati katika kuitumikia kada hii, ambayo ni
mojawapo kati ya kada muhimu na zinazoheshimika duniani na tunaahidia
kuendelea kuwapa ushirikiano wetu katika kufanikisha jitihada na maono
yao.
Mwisho, kama alivyosema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bibi. Hillary Clinton, ni lazima tukumbuke kuwa katika maeneo mbalimbali duniani bado waandishi wa habari wanakabiliwa na vitendo vya unyanyasaji, ukatili na wakati mwingine kuuawa.
Leo
hii tunakumbuka kuwa uandishi wa habari ni wito wa mashujaa wa kila
siku. Ni lazima tuendelee kusimama kidete na kuwatetea wale wanaosimama
na kupaza sauti zao katika mazingira hatari wanapotekeleza wajibu wao wa
kutafuta, kurekodi na kufichua ukweli.
Dana L. Banks
Afisa wa Masuala ya Umma
Ubalozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)