UDOM SOCIAL YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NA KUNYAKUA KOMBE KATIKA LIGI YA MPIRA WA KIKAPU DODOMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

UDOM SOCIAL YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NA KUNYAKUA KOMBE KATIKA LIGI YA MPIRA WA KIKAPU DODOMA

Nahodha wa timu ya mpira wa kikapu kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) akipokea kombe la ushindi wa timu yake UDOM Social  kutoka kwa Mgeni rasmi pichani kati,Diwani wa kata ya Mnadani,Mh.Steven Masangia mara baada ya kuibuka kinara kwenye ligi ya mashindano ya mpira wa kikapu iitwayo DODOMA BASKETBALL DEVELOPMENT LEAGUE 2012,ambayo imefikia tamati leo kwenye uwanja wa mchezo huo uliopo ndani ya uwanja wa mpira wa miguu wa Jamuhuri mjini Dodoma
Nahodha wa timu ya mpira wa kikapu kutoka chuo cha MIPANGO-Dodoma akipokea kombe la ushindi wa timu hiyo kutoka kwa Mgeni rasmi pichani kati,Diwani wa kata ya Mnadani,Mh.Steven Masangia mara baada ya kuibuka mshindi wa pili kwenye ligi ya mashindano ya mpira wa kikapu iitwayo DODOMA BASKETBALL DEVELOPMENT LEAGUE 2012,ambayo imefikia tamati leo kwenye uwanja wa mchezo huo uliopo ndani ya uwanja wa mpira wa miguu wa Jamuhuri mjini Dodoma
 Pichani kati ni  Mgeni rasmi na Diwani wa kata ya Mnadani,Mh.Steven Masangia akizungumza mapema leo jioni mara baada ya kuisha kwa fainali ya ligi ya mchezo wa kikapu iitwayo DODOMA BASKETBALL DEVELOPMENT LEAGUE 2012,ambayo imefikia tamati leo kwenye uwanja wa mchezo huo uliopo ndani ya uwanja wa mpira wa miguu wa Jamuhuri mjini Dodoma Ligi hiyo ilizishirikisha timu tisa,ambazo ni UDOM,Chuo cha Mipango Dodoma,St.John,CBE,Don-Bosco,Dom Warriors,Dom Spears,Dodoma Spurs pamoja na UDOM Education
Wachezaji wa timu ya UDOM-Social wakilisakama vilivyo goli la timu ya chuo cha MIPANGO.
  Mchezaji wa timu ya UDOM-Social akitaka kumtoka mchezaji wa timu ya MIPANGO.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages