Mkurugenzi
mkuu wa NHC na mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo
Nehemia Kyando Mchechu, akitoa taarifa yake kwa wajumbe wa baraza hilo
(hawapo pichani). Kulia ni naibu katibu mkuu wa wizara ya ardhi, nyumba
na maendeleo ya makazi Maria Bilia.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Maria
Bilia, akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa NHC. Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Kyango Mchechu na kulia ni Katibu baraza
la wafanyakazi wa NHC Erasto Chilambo
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa NHC wakifuatilia kwa makini ajenda za baraza hilo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Maria
Bilia (kulia) akiongozana na mkurugenzi mkuu wa NHC,Nehemia Kyando
Mchechu, kuingia kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kufungua kikao
cha baraza la wafanyakazi wa NHC nchini.
Jengo
la Lake Hill Hotel la mjini Singida mahali kikao cha baraza la
wafanyakazi wa NHC kinafanyika.Picha zote na Nathaniel Limu
--
Na Nathaniel Limu.
Shirika
la nyumba la Taifa (NHC) limehimizwa kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba
za kuuza na hasa za gharama nafuu, kama njia mojawapo ya kuisaidia
serikali kupambana na vita dhidi ya umaskini.
Akifungua
kikao cha baraza kuu la wafanyakazi wa NHC nchini Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Madeye (MB) amesema
serikali inaamini kuwa mkiongeza kasi zaidi katika ujenzi wa nyumba,
licha ya kuwa mtakuwa mmetekeleza ilani ya uchaguzi ya chama tawala, pia
mtaisaidia serikali katika juhudi zake za kuondoa umasikini nchini.
Amesema
kuwa serikali kwa upande wake, inaendelea kujitahidi kuboresha sera ya
nyumba na sheria mbalimbali ili kufanya sekta ya nyumba hapa nchini
iweze kuchangia kikamilifu pato la taifa.
Katika
hatua nyingine, Madeye amesema hivi sasa kuna ushindani mkubwa katika
sekta ya nyumba hapa nchini, pamoja na ushindani huo, NHC haina budi
kutambua kuwa wanalo jukumu la kuhakikisha wanawasaidia Watanzania
wote, kumiliki nyumba bora.
Awali
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Kyando Mchechu, amesema wameweza
kuboresha mambo mengi makubwa katika shirika hilo, ikiwemo uboreshaji wa
ukusanyaji mapato kutoka shilingi bilioni 2.9 kwa kipindi cha mwaka
jana,hadi shilingi bilioni 4.7 kwa sasa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)