Baadhi ya wanachama wa Yanga wakifanya
fujo klabuni hapo kupinga mkutano wa waandishi wa habari uliokuwa
ufanywe na mwenyekiti wa klabu hiyo Bw. Loyd Nchunga leo mchana ambapo
polisi walifika klabuni hapo na kuimarisha ulinzi hadi Fullshangweblog
inaondoka klabuni hapo bado kulikuwa na kundi la wanachama na kila moja
akiongea la kwake na mkutano ulikuwa bado kufanyika.
Mmoja wa askari akimuondoa mmoja wa wanachama wa klabu hiyo katika eneo lililokuwa na vurugu klabuni hapo.
Polisi wakiwa katika magari yao tayari kabisa kuzuia vurugu endapo zingezuka klabuni hapo.
Moja wa magari ya polisi likiwa limeegeshwa nje ya klabu hiyo kwa ajili ya kulinda usalama klabuni hapo leo mchana.CREDITS: FULL SHANGWE BLOGU |
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)