Mkopo
huo umetolewa na PPF kwa Mwauwasa Saccos ni moja ya huduma
zinazotolewa na PPF na wanachama wake ili kuwawezesha kiuchumi na
kuwaondolea ugumu wa maisha unaotokana na kukosa kipato cha kutosha na
pia kuwaandaa waweze kuwa na maisha bora wawapo katika ajira na mara
baada ya kustaafu.
"Huu
ni mpango mahususi wa PPF katika kuboresha maisha ya wanachama wake,
mpaka sasa PPF imekwishatoa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 40 kwa
vyama vya kuweka na kukopa 36 kwa nchi nzima , na lengo la utoaji wa
mikopo hiyo ni kuwawezesha wanachama wa PPF katika ujenzi wa nyumba,
kulipa gharama za elimu, kujiendeleza katika kilimo, kujiendeleza
kibiashara na kuwa na ufugaji bora”, alisema Meshack Bandawe (Pichani).
Mwenyekiti wa Mwauwasa Saccos, Vedastus Pilla (Pichani) ameushukuru
uongozi wa PPF kwa uamuzi iliouchukua ya kuiweza Mwauwasa Saccos ili
iweze kuimarika kiuchumi na kuwawezesha wanachama wake kupata maisha
bora.
Meneja
wa MWAUWASA Saccos, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa mfuko
wa PPF pamoja na wanachama wa chama hicho cha kuweka na kukopa cha
Mamlaka ya Maji safi na majitaka jijini Mwanza, muda mfupi baada ya
kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni 900 za mkopo kwa
wanachama wa saccos hiyo leo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)