Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Charity Food Products ya Mwanza
Sophia Kagose (kushoto ) akionyesha mifuko ya dagaa waliokaagwa njisi
walivyo sindikwa kwa utalaam katika maadhimisho ya Siku ya Afrika
yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kulia
ni Meneja wa kampuni hiyo Favour Dietrich.
Adelina Aloyce ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya ADE FASHION Designer
akiwaonyesha moja ya nguo zake wateja waliofika katika banda lake katika
maadhimisho ya Siku ya Afrika yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Equator Natural Cosmetics Mrs Liwa akiwaonyesha wateja
wake waliofika katika banda lake jinsi ya kutumia Lotion ya kitanzania
inayojulikana kwa jina Sanda Luwood, ambayo inatumika kwa kulainisha
ngozi vizuri katika maadhimisho ya Siku ya Afrika yanayoendelea katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Kampuni ya Designer Glass Beads Febronia Mihuwa akimuonyesha
Tula Mkemwa njisi ya kumechisha shanga ya shingoni na mkoba wakati
alipotembelea katika banda lake katika maadhimisho ya Siku ya Afrika
yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Kwa hisani ya Full Shangwe Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)