Maandamano ya
wafanyakazi wa Mashirka na Taasisi mbalimbali yakipita kwenye makutano
ya barabara ya Msimbazi na Morogoro, leo wakati yakitokea Viwanja vya
Kidongo Chenkundu kwenda Mnazi Mmoja kwenye maadhimisho ya Siku ya
Wafanyakazi Duniani aka MEI MOSI.
Wafanyakazi wa
kampuni ya TSN, wachapishaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News,
Habari elo na Spoti Leo wakiwa na bango lao kwenye maanamano hayo
Wafanyakazi wa TSN walkionyesha furaha wakati wakiwa kwenue matembezi hayo
Wafanyakazi wa TSN
Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHF) wakiwa kwenue maandamano hayo na miavuli yenye nembo ya Taasisi hiyo.
Wafanyakazi wa NHF
Mahakama nao hawakubaki nyumba kwenye maandamano hayo
Wakati baadhi ya Watanzania wanalia na wawekezaji Wafanyakazi wa Swussport wao wanasema wawekezaji siyo wabaya ila....
Hawa nao ni wafanyakazo wa taaisi moja, wakikimbia na bango lao kuwahi Mnazi Mmoja
Wengi wamejitokeza katika kuhakikisha Siku yao ya wafanyakazi inanoga
Tafadhali soma ujumbe wa wafanyakazi hawa.
Kutokana na
maandamano hayo magari yalilazimika kusubiri kwa zaidi ya dakika 25
kwenye taa za kuongozea magari katika makutano ya barabara ya Morogoro,
kiasi kwamba kodakta wa daladala moja alipata fursa ya kwenda ku-chati
na Trafiki (kushoto) kama walivyonaswa na kamera yetu.Picha kwa Hisani ya Bashir Nkoromo Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)