Counsellor
of the high commiission of India Mr. Kunal Roy addressing the media
during the media briefing of the indiafrica shared future proogramme.
on his right if semma kunda director of theideaworks.
The
Marketing Director at The University of Dar es Salaam Dr. Omary Mbura,
talking to the press during the INDIAFRICA press conference.
The
creative Entrepreneur Mustafa Hassanali, talking to the media during
the Media briefing of the INDIAFRICA A Shared future programme.
Ms.
Seema Kundra, The Director of the theIdeaWorks, presenting The
INDIAFRICA A Shared future presentation during the media briefing of The
INDIAFRICA Programme.
---
Mpango maalumu wa nchi ya India wa kukuza mbinu za ushirikiana wa kinaendeleo baina ya India na Afrika
Kwa
mujibu wa Balozi Pinak Chakravarty, Katibu Maalumu wa idara ya Umma ya
Wizara ya Mambo ya Nje na Diplomasia "India na Afrika tunaingia katika
ukurasa mpya baada wa kihistoria kupitia ukoloni na unyonyaji wa
kiuchumi hadi kufikia uhuru. Na sasa uhusiano wetu unazidi kukua kwa
kasi. Uhusiano wetu huu mpya umeegemea zaidi katika uhusiano wa kiuchumi
katika dunia hii ya utandawazi.
theIdeaWorks,
ni mpango maaalumu wa kibiashara ambao makao makuu yake yako mjini
Delhi, na unasimamiwa na idara maalum ya Umma, chini ya Wizara ya Mambo
ya Nje ya serikali ya India. INDIAFRICA: A Shared Future ni mpango wa
miaka mitatu na ulizinduliwa mnamo mwaka 2011.
Mpango
wa P2P inakaribisha mbadilishano wa mawazo kati ya vijana kutoka Africa
na India, kupitia mfululizo wa mashindano mbalimbali ya wajasiriamali
vijana. Pia ina lengo la kujenga jukwaa la vijana wajasiriamali kutoka
India na Afrika lenye nguvu, uvumbuzi na ushindani.
"Kuongezeka
kwa uwezo wa kiutamaduni, ni muhimu kwa ajili ya mafanikio, Na
kuwajenga vijana kuwa raia wazuri wa kimataifa na kukuza ndoto na
matarajio yao katika nchi yoyote duniani. Kwa mtazamo huu, watu hasa
vijana wana jukumu kubwa na muhimu la kujenga dunia na kushikamana ili
kuweza kuleta maisha bora kwa watu wote baadae, ikiwa watu wote bilioni
mbili wakijenga ndoto na historia yao kwa pamoja." Alisema Seema Kundra,
Mkurugenzi wa theIdeaWorks.
INDIAFRICA:A
Shared Future ni mpango wa kimawasiliano unaojumuisha mashindano
mbalimbali kama, uandishi wa insha, upigaji picha na ubunifu. Hii
itasaidia kujenga jukwaa la vijana kutoka Afrika na India wenye vipaji
na uwezo wa kushirikiana katika changamoto na mafanikio yao; Na baadae
kushirikiana kiubunifu, biashara na utamaduni.
Jumuia
ya vijana wenye malengo na mipango ya kubainisha wajasiriamali vijana
kutoka India na Afrika, na unawapa fursa ya ukuaji na ushirikiano. Lengo
lake ni kubadilishana mawazo na kuongeza uelewa mzuri wa changamoto na
fursa za kibiashara katika pande zote mbili.
Nikimnukuu
Navdeep Suri, Katibu Mkuu wa Idara ya Diplomasia na Umma, Wizara ya
Mambo ya Nje ya India alisema, "70% ya idadi ya idadi ya watu katika
bara la Afrika kwa sasa wako chini ya umri wa miaka 25, ambapo ni
takwimu zinazoshabiihana na India. Hivyo basi ni muhimu sana kukuza
ushirikiano kati ya vijana kutoka Afrika na India ili kusafisha njia kwa
ajili ya malengo ya pamoja hapo baadae. Lengo la mpango huu ni kufanya
kazi kwa pamoja ili kuibua nishati hiyo kubwa ya vijana na kuhamasisha
mawazo yao ya kipekee na yenye nguvu na ubunifu, na kuwawezesha kuwa
wawezeshaji na vichocheo vya mchakato huo."
Katika
kila kila kundi la ushindani, zawadi ya fedha taslimu ya Dola 1000 za
Kimarekani kwa washindi watatu kutoka kila kanda ambazo ni Afrika
Mashariki,Afrika Magharibi,Afrika ya Kati,Kusini na India.
Kila
mshindi wa shindano la vijana wenye maono, watapewa ziara ya siku tano
kati ya India au Afrika (kulingana na nchi aliyopo) ambayo itaambatana
na semina na mikutano ya kibiashara; Pamoja na muingiliano ya
kimawasiliano ya kibiashara. Washiriki wachache wa mwisho watakaotajwa
wataweza kushiriki katika shindano la dola 10,000 za Kimarekani na
kuendeleza ushirikiano kati ya India na Afrika.
INDIAFRICA
itasaidia kuvunja mipaka na kukuza na kuhamasisha ushirikiano mpya, na
utambuzi wa kimataifa na kutatua matatizo ya kirasilimali kati ya
wanafunzi wa vyuo vikuu, shule za sekondari,sekta ya viwanda,
wajasiriamali na viongozi kutoka India na Afrika ili kuweza kuukaribisha
mpango huu wa INDIAFRKA.
Hivyo
kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambao kwa sasa
wanasherehekea miaka 50 ya kuanzishwa kwake pamoja na AIESEC
Tanzania,INDIAFRICA imeandaa kongamano linalojumuisha vyuo vyote
litakalofanyika mnamo tarehe 12 Mei 2012 katika ukumbi wa Nkuruma ndani
ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kongamano hili ni bure kabisa kwa
wanfunzi wote wa elimu ya juu, wataalamu na vijana. Washiriki wote
watapata nafasi ya kubadilishana mawazo na wajasiriamali vijana kutoka
India na Tanzania.
"Mpango
huu ni jukwaa kamili la kwa ajili ya wajasiriamali vijana, kwa ajili ya
kuandaa matarajio yao ya baadae ya kazi zao. Maendeleo yetu ya kesho,
yamo mikononi mwa kijana wa leo, nami nimepata heshima ya kuwa sehemu ya
mradi huu ambao una lengo la kuleta India na Afrika kwa pamoja hasa
Tanzania ; Kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili kwa karne mbili"
Alisema Mustafa Hassanali mbunifu nguli wa mavazi Tanzania na muandaaji
wa Swahili Fashion Week.
Swahili
Fashion Week kwa pamoja na INDIAFRICA wanaandaa mashindano maalumu kwa
ajili ya kuleta muingiliano kwa vijana wadogo wanaochipukia katika
nyanja ya ubunifu wa mitindo nchini Tanzania, ambapo washindi wataweza
kuonyesha ubunifu wao katika maonyesho makubwa ya mavazi Afrika
mashariki na kati ya Swahili Fashion Week yanayofanyika mwezi November
kila mwaka.
"Tunatoa
wito mkubwa kwa kila mtu kushiriki katika mdahalo huu wa aina yake hapo
tarehe 12 Mei 2012,ambapo hautapata nafasi ya kukutana na vijana
wajasiriamali wenye maono ya mafanikio na maendeleo tu, bali pia hafla
fupi ya muziki itakayofanywa na wasanii wanaotikisa nchini Tanzania,"
Alihitimisha Seema Kundra
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)