Nahodha wa
timu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Charles Evance akipokea kitita cha
pesa Shilingi Laki tano kutoka kwa Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Kinondoni,
Jumanne Mlimi maaara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wakati mashindano ya
Pool Safari Higher Learning yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.
Wachezaji
wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya ushindi wa kwanza Shilingi
laki tano kutoka kwa kwa Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Mlimi
maaara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wakati mashindano ya Pool Safari
Higher Learning yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
IFM MABINGWA
SAFARI HIGHER LEARNING DAR
CHUO cha
usimamizi wa Fedha cha Dar es Salaam(IFM) wametetea ubingwa wao juzi katika
mashindano ya Pool Safari Lager Higher Learning yaliyomalizika kwenye Ufukwe wa
Coco Beach jijini Dar es Salaam.
IFM
waliutwaa ubingwa huo kwa kuwachapa majirani zao chuo cha Elimu ya
Biashara(CBE) 4-0,hivyo kujitwalia tena ubingwa kwa mara ya pili kwa Mkoa wa
Dar es Salaam na kuibuka na zawadi ya kitita cha Shilingi laki tano
Mshindi wa
pili katika mashindano hayo ni CBE ambao walizawadiwa laki tatu,wapili ni Chuo
cha Ardhi ambao walipata laki mbili na wanne ni Chuo cha DIT ambao walipata
laki moja.
Wachezaji wa
singles(mmoja mmoja) wanaume alishinda Peter Patrick kutoka chuo cha IFM
alinyakua ubingwa akifuatiwa na Goodhope Mamkwe kutoka IFM pia,wakati upande wa
Wanawake bingwa alikuwa Modesta David kutoka IFM akifuatiwa na Lilian Meiri
kutoka chuo cha CBE.
Mshindi wa
kwanza wa singles (mmoja mmoja) wanaume, Peter Patrick akionyesha zawadi yake
mara baada ya kukabidhiwa na Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Kinondoni, Jumanne
Mlimi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wakati mashindano ya Pool Safari
Higher Learning yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa
kwanza wa singles (mmoja mmoja) wanwake, Modesta David akipokea zawadi yake
kutokan kwa Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Mlimi mara baada ya
kuibuka washindi wa kwanza wakati mashindano ya Pool Safari Higher Learning
yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Msindi wa
kwanza wa singles (mmoja mmoja) wanawake, Modesta David akionyesha zawadi yake
kwa furaha mara baada ya kuibuka mshindi wakati wa mashindano hayo ya Pool
Safari Higher Learning yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
VYUO 8 VYA
ELIMU YA JUU USO VYAFUZU KUSHIRIKI FAINALI ZA SAFARI POOL.
VYUO vinane
vimefaulu kuingia katika fainali za mashindano ya Pool Safari Higher Learning
yatakayofanyika Mkoani Iringa May 26 mwaka huu kutoka katika Mikoa minane.
Akizungumza
mratibu wa mashindano hayo, Michael Machellah vyuo vilivyofaulu kuingia katika
fainali hizo ni Morogoro ni Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kilimanjaro ni Chuo cha Ushirika Moshi(MUCCOBS), Dodoma ni
St.John,Arusha ni Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Mwanza ni St.Augustine,Iringa
ni Ruaha(RUCO),Mbeya ni Chuo cha
Uhasibu(TAA) na Dar es Salaam ni Chuo
cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Wachezaji wa
singles(mmoja mmoja) wanaume na wanawake kila mkoa watawakilishwa na mabingwa
wa kila mkoa ambapo Morogoro ni Moyo Hamza kutoka Chuo cha Ardhi na Fotunate
Shija kutoka chuo cha SUA,Kilimanjaro ni Alphael Jackson kutoka MUCCOBS na
Suche Anastasia kutoka KCMUCO ,Dodoma ni justace Mhando kutoka MIPANGO na Lemi
Jackson kutoka U-DOM na Waku ,Arusha ni Vicent Katiyega kutoka chuo kikuu cha
Arusha(UOA) na Violeth Silas kutoka IAA ,Iringa ni Said Mohamed kutoka RUCO na
Beatrice kutoka RUCO, Mwanza ni Joachim Mushi kutoka CBE na Agnes Mtalika wa
chuo cha Bugando,Mbeya ni na Dar es Salaam ni Feter Patrick kutoka chuo cha IFM
na Modesta David kutoka IFM.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)