HISTORIA FUPI YA WAPI BLOGS ZIMETOKA NA MPAKA KUJIPATIA UMAARUFU DUNIANI KOTE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

HISTORIA FUPI YA WAPI BLOGS ZIMETOKA NA MPAKA KUJIPATIA UMAARUFU DUNIANI KOTE

Blog ni neno lililotokana na neno (web log) ni makala ya mtu mmoja inayochapishwa kwenye www (World Wide Web) ambayo inahusisha posts au makala. Makala hizo zinazokuwa zinachapishwa kwenye mtandao  zinakuwa kwenye mpangilio maalumu na zinaonyeshwa kwenye mpangilio maalumu ambapo post ya kwanza ndio inaonekana kuwa latest au habari mpya (recent). Blog mara nyingi ni kazi inayofanywa na mtu mmoja (individual), au sehemu ya kazi ya group dogo la watu kuhusiana na jambo flani na inakuwa na lengo flani. Neni Blog linaweza kutumika kama kumaintaini au kuongeza vitu (Contents) kwenye mtandao
Blog zimeanza kwa kasi katika miaka ya mwisho mwa 1990 huku ikihusika na kuweka au kuchapisha machapisho kwenye tovuti ambapo huweza kufanywa na kila mtu hata ambaye siye mtaalamu wa maswala ya tovuti. Mwanzoni elimu hiyo ilikua ikijulikana kama HTML (Hyper Text Markup Language) na File Transfer Protocal (FTP) kwa kiswahili mpangilio wa kutuma file kwanjia maalum katika kuchapisha habari (Content) katika tovuti.
Japokuwa Sio lazima, Na Ubora mkubwa wa blog ni muingiliano, kuruhusu watembeleaji kuweza kuacha maoni yao na hata ujumbe wa maneno kupitia GUI (Graphic User Interface) kitufe cha mtumiaji katika blog hizo na kutofautisha blog hizo na tovuti nyingine. Kwa maana hiyo Blogs imeonekana kuwa ni Mtandao wa Kijamii. Hata hivyo wanoendesha blog hizo (bloggers) sio tu wanaweza kuweka post kwenye mtandao huo bali pia hutengeneza mahusiano na wasomaji wao na waendeshaji wenzao wa mitandao hiyo.

Blog nyingi zimekuwa zikiweka au kutuma makala kuhusiana na habari mbalimbali juu ya kitu flani, na matumizi mengine ya blog ni kwamba blog ni moja ya kitabu cha mtandaoni cha kumbukumbu ya mtu vilevile blog zimekuwa sehemu mojawapo ya chombo cha matangazo ambapo kampuni au mtu binafsi anaweza kutangaza biashara yake au bidhaa zake

Blog za Kawaida kabisa zinahusisha Maneno, Picha na viunganishi (links) za kwenda kwenye tovuti nyingine au mitandao mingine, Kurasa za tovuti na media nyingine zinazohusiana na mada husika. Uwezo wa Wasomaji katika kuacha maoni katika muundo muhimu ambao ni sehemu ya blog nyingi.

Blog nyingi zipo kwenye mfumo wa Maneno, japokua malengo ni kuonyesha fani ya sanaa (art Blog), Blog za Picha(Photoblog), Video blog(Video blogging or vlogging), muziki blogging (MP3 Blog) na Blog za Sauti (Podcasting)

Mpaka kufikia tarehe 16 Mwezi wa 2 mwaka 20122 kulikua na blog za umma zipatazo Milioni 156  

HISTORIA YA BLOG.

Neno Weblog liliunganishwa na mtaalamu aitwaye John Barger mnamo tarehe 17 Disemba 1997. Kifupi cha Neno Blog kilitengenezwa na mtaalamu aitwaye Peter Merholz ambaye alivunja neno Weblog katika maneno mawili "We Blog" katika upande wa pili wa tovuti yake ya Peterme.com ambayo aliianzisha mnamo April au May 1999.

Baada ya Hapo Evan Williams kutoka Maabara ya Pyra alitumia blog kama neno na kitendo cha kurekebisha weblog ya mtu mmoja au kutuma habari kwenye weblog ya mtu pia. 

UZALIWA WA BLOG

 Kabla ya kuwa na blog hakujawa maarufu, jumuiya ya mfumo wa namba (Digital Communities) ilichukua aina nyingi ya mfumo kama vile Usenet, Huduma za Biashara za mtandaoni kama vile GEnie, BiX na mwanzoni CompuServe, na listi ya barua pepe (e-mail lists) na Bulletin Board Systems (BBS). 

Blog ya kisasa ilihusisha kumbukumbu ya mtu mtandaoni (Online Diary), ambapo watu waliweza kuendesha akaunti  zao mtandaoni na kuweka taarifa za maisha yao. Waandikaji wengi wa mitandaoni waliweza kujiita diarist, waandishi wa habari na waandika makala. Mnamo mwaka 1994 Mwanafunzi ajulikanaye kama Jerry Pournelle kutoka Chuo Cha Swarthmore aliweza kujulikana kama ni mmoja wa waendesha blog wa mwanzo kabisa wakati huo Dave Winer's muandika miongozo ya habari (Scripting News) alikua mtu aliyetajwa kuwa mkongwe na mtu wa muda mrefu kuendesha weblog

Blog nyingine ya mwanzo ilikua Wearable Wireless Webcam ambayo ilikua ni mtandao unaoshea habari,taarifa za maisha ya mtu ikihusishwa maandishi, video, na picha ambazo zilitumwa moja kwa moja kwa wearable computer na kifaa cha jicho (Eye Tap)kwenda kwenye mtandao au tovuti mnamo mwaka 1994

Zoezi hili la kuposti habari na taarifa kwenye blog moja kwa moja kupitia video pamoja na maandishi kulijulikana kama sousveillance, na makala hizo ziliweza kutumika kwenye maswala ya kisheria kama ushahidi

Baadhi ya Waendesha blog wa mwanzoni kabisa kama  Misanthropic Bitch,ambaye alianza mnamo mwaka 1997, aliweza kujulikana kwa kuwepo hewani kama  zine, kabla ya neno blog kuingia katika matumizi ya kawaida.

KUKUA KWA UMAARUFU WA BLOG

Baada ya mwanzo mdogo, Kuwa na blog au kuendesha blog ghafla kuendesha blog kukapata umaarufu. Matumizi ya blog yakaanza kusambaa kuanzia mnamo 1999 na miaka iliyofuata blog zikaanza kuwa maarufu na aliyeendesha blogu pia waliweza kuwa maarufu mpaka karibia na kuwasili kwa vifaa vya kwanza vya kubeba blog (Hosted Blog tools)

Mtaalamu ajulikanaye kama Bruce Ableson alizindua kitabu chake cha kumbukumbu mtandaoni mnamo mwaka  1998 na muda mfupi baadae kitabu chake hiko kikaweza kukua na kugundua maoni ya wasomaji na blog yake hiyo kuwa blog ya kwanza ya jumuiyaambapo wasomaji waliweza kutoa maoni kwa waandikaji wengine

Mtaalamu mwingine Brad fitzpatrick alianzisha makala ya Moja kwa Moja (LiveJournal) mnamo mwezi wa 3 mwaka 1999 

Andrew Smales naye alitengeneza Pitas.com mnamo mwezi wa 7 mwaka 1999 ikiwa kama njia mbadala na rahisi katika kumaintaini kurasa za habari katika tovuti na kufuatiwa na Diaryland mnamo mwezi wa 9 mwaka 1999

 Mnamo Mwezi Wa 8 Mwaka 1999 Evan William na Meg Hourihan kutoka maabara ya Pyra walizindua tovuti ambayo ndio inaendesha na kubeba blog zote ijulikanayo kama blogger.com. Na Mnamo Mwezi wa 2 mwaka 2003 Kampuni ya Google ikanunua Injini ya kuendeshea Blog yani blogger.com

Mnamo mwaka 2004 , umuhimu wa blog ukaanza kuongezeka kama vile ushauri wa kisiasa, huduma za habari na watahiniwa walianza kutumia blog kama kifaa kwaajili ya kuwafikia watu na sehemu ya kutoa maoni.

Kuendesha blog kulianzishwa na wanasiasa na wagombea katika kueleza mitazamo yao,maoni yao kuhusiana na vita na mambo mbalimbali na kuziimarisha blog kuwa chanzo cha habari
Mnamo Mwezi wa kwanza mwaka 2005 Gazeti la Fortune lilitaja waendesha blog nane wafanyabiashara ambao hawewezi kukataa kufanya kazi hiyo ambao ni Peter Rojas, Xeni Jardin, Ben Trott, Mena Trott, Jonathan Schwartz, Jasom Goldman, Robert Scoble na Jason Calacanis

Nchi ya Israel Ni Moja ya Nchi ya Kwanza Kutengeneza na kumiliki Blog ambayo ilikua chini ya David Saranga ambaye alikua Waziri Wa Mambo ya Nje na alikua makini katika kuzoea Web 2.0 na kuendeleza video blog na Blog ya Siasa

Waziri huyo Wa Mambo ya Nje aliweza kumiliki aina ndogo ya Blog (microblogging) na kuweza kufanya mkutano na waandishi wa habari kupitia tovuti ya Twitter kuhusiana na vita vyake na Hamas, pamoja na Saranga kujibu maswali kutoka kwa umma 

Maswali na majibu juu ya blog yaliweza kuwekwa katika Blog ya Siasa za Israel.

AINA ZA BLOG:

Kuna aina nyingi za blog achilia mbali vinavyoandikwa hata mpangilio wa maandishi katika mada flani.

Kuna blog ya mtu binafsi ambapo mwenye blog anaweza kuweka taarifa zake zinazomuhusu yenye mwenye au kuchagua anachotaka kuweka katika blogu  yake husika

Blog za Mashirika Na Makampuni hizi ni blog zinazomilikiwa na shirika au kampuni flani ambapo kampuni au shirika hilo hutumia blog hiyo kuweza kutangaza huduma na bidhaa zake
Vilevile Blog zimekua kama chombo kimoja wapo cha kuweza kutangaza biashara na kuwa njia ya kujipatia kipato kwa muendeshaji wa blog husika na umaarufu wa blog umeweza kuanzisha kitu kinaitwa fake blog fake blog ni blog zinazofunguliwa na kampuni kwaajili ya kutangaza bidhaa zake tu

Vilevile Blog imeweza kuwa sehemu ya kutengeneza ajira endapo mtu anamiliki blog na kuifanya kama kazi inaweza kumpatia kipato kikubwa na kuweza kuendesha maisha yake kupitia blog na makampuni mengi sahivi yameweza kuwachukua waendesha blog katika kazi kwasababu ya uharaka wa habari kitu ambacho kinafanyika muda huu basi kinaweza kuonekana mara moja endapo mwendesha blog hataweka taarifa hiyo muda huo huo lakini pia ni njia moja wapo ya haraka sana katika kufikisha habari kuliko media nyingine yoyote.

Waendesha blog wengi wameweza kupata ajira na kujiongezea kipato kutoka na makampuni mengi kuona tija ya kuweza kutangaza bidhaa zao na huduma zao kupitia blog kwasababu habari hiyo huweza kuwafikia watu ndani ya muda mfupi na watu kuweza kuona habari hiyo.

Makala Hii Imeandaliwa na Josephat Lukaza Kwa Msaada wa Vitabu na Mtandao kutoka Tovuti Mbalimbali

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages