Hivi ndivyo Fuso hilo lilivyokuwa baada ya ajali
Wananchi na polisi wakisaidiana kuinasua miili ya watu watatu walio kufa katika ajali
Mwili wa dereva Taxi ukiwa bado kutolewa
Wananchi na polisi wakisaidiana kuinasua miili ya watu watatu walio kufa katika ajali
Wananchi wakitazama Fuso ambalo liligongana na Taxi hiyo
Askari
wa usalama barabarani mjini Iringa wakiwa wamebeba moja kati ya maiti
za ajali ya Taxi na Fuso iliyotokea eneo la kituo cha Mafuta Eso kwenye
barabara kuu ya Iringa -Mbeya asubuhi hii
Miili ya wafanyakazi wa barabara Iringa ambao walikufa katika ajali hiyo
Ajali
mbaya imetokea mjini Iringa asubuhi hii na kusababisha vifo vya watu
watatu papo hapo huku abiria waliokuwemo katika fuso wakinusurika
katika ajali hiyo .Mashuhuda waliozungumza na Mdau
Francis Godwin wamedai
kuwa Taxi hiyo yenye namba za usajili T620 ANE ilikuwa ikitokea Ndiuka
ikiwapeleka wafanyakazi wa barabara katika eneo la Tanangozi am,bako
ujenzi wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya uinaendelea .
Hata
hivyo kabla ya kufika katika eneo hilo la kituo0 cha Mafuta cha Eso
dereva wa Taxi hiyo ambaye alikuwa akitaka kulipita gari jingine
lililokuwa mbele yake alishindwa kulipita gari hilo baada ya kukutana
uso kwa uso la Fuso yenye namba za usajili T897 AQS ambalo lilikuwa
limeshehena magunia ya mpunga .
Hivyo
kutokana na mwendo kasi ambao Fuso hilo lilikuwa likienda nao na
mwendo kasi wa Taxi hiyo uwezekano wa kukwepana ulishindikana na hivyo
kupelekea fuso hilo kuigonga Taxi hilo na kuipitia kwa juu na kupelekea
vifo vya abiria wawili na dereva wa Taxi hiyo papo hapo .
Jitihada
za kuzitoa maiti hizo zinaendelea hadi sasa japo eneo la tukio likiwa
limetapakaa ubongo wa maiti hizo za ajali na wasamaria wema wakiendelea
kufanya kazi hiyo ya kuzitoa maiti bila ya kutumia kinga yeyote na
hivyo idadi kubwa ya wasamaria wema hao waqmeonekana wakiwa wametapakaa
damu .
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)